NaimaOmari
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 801
- 50
Wapendwa wana JF naombeni msaada wenu katika hili;
Mimi nipo kwenye ndoa ni mwaka mmoja sasa lakini matatizo ndani ya hii ndoa hayaishi.Mimi na mme wangu wote tunafanya kazi ila kuna mambo nashindwa kuyaelewa na ninabaki njia panda!
Mwezi uliopita nilikwenda likizo nyumbani cha ajabu wakati najiandaa kuondoka asubuhi mme wangu akaninyang'anya card yangu ya benki eti akifikiria nitakwenda kuwapa pesa nyumbani kwetu!
Kwa kweli tulibishana sana hadi nikafanikiwa kuondoka na card yangu ila alikasirika sana hadi akasema nikirudi nije na wazazi wangu eti hanitaki tena!
Nimeenda likizo nimerudi yakawa yameisha cha ajabu tukawa tumetoka out na waliokuwa washenga wetu wa harusi acha aanze kusimulia yaliyotokea!
Mimi ninaamini katika kusamehe na kusahau lakini mwenzangu ukifanya kosa anakumbushia na makosa yaliyopita nashindwa kuelewa ni kwa nini?
Kwa kweli mimi inaniuma sana na kuna kipindi najiuliza hivi kweli huyu mme wangu ananipenda kweli?
Naombeni mnisaidie katika hili kutokana na hizi tabia za mme wangu mimi nifanye nini?
Amelie!
Oa wewe! Usiogope elimu ya mwanamke. Usiparamie wanawake, tafuta mke. Wanawake ni wengi lakini wa kuwa mke ni mmoja naye akija huna ujanja huo wa Mwana-FA! It's the matter of time.
Mkuu unaona sasa ishu hii ya Amerie yeye hataki kujishusha ndo maana jamaa anakuwa mbogo.Lakini akijifanya mjinga mambo yanakuwa shwali kabisa.
Lakini ni wachache sana ambao wana roho za kujishusha lakini ukipata mwanamke mwenye Masters au PHD na kwendelea huko wewe una kabachara au kadiploma mkuu walahi nyumba itakuwa ndogo hapatoshi.....mmh mimi bado nipo nipo kwanza nyie tangulieni kwanza...
Amelia pole sana .. this is the true him resurfacing .. guess you still have a lot to learn from him
You better show him your stand now otherwise ukikubali from the beginning then thats it you have no time to raise your head again kwani the next step ni beating
Amelie,
Ngoja nijaribu kuwa mshauri wenu kidogo...
Matatizo ya namna hii hayakuandami wewe pekee, wapo wengi wa namna yako.
Amelie, wewe ni mkristu? Mkatoliki? Mlienda semina ya ndoa kabla ya kufikia maamuzi ya kufunga ndoa kanisani? Kama si mkatoliki basi uliikosa fursa hii ya kipekee ambapo ungemsikiliza mfundishaji ungeweza kuchukua maamuzi kabla ya kuingia katika ndoa ambayo kwa mwaka mmoja tu unaanza kuhisi ni ndoano.
Ndoa ni kitu cha heri kabisa na wala usikijutie, kughafirika ni kwa kila binadamu na kubadilika inawezekana!
Kwanza:
Kuna ilani mliyojiwekea kuhusiana na masuala ya benki? Simu? Akaunti za barua pepe n.k? Kama hapana basi hili ni tatizo ila hujachelewa, mnaweza kuelewana mapema tu juu ya nini kifanyike na kivipi.
Pili:
Una kawaida ya kugawa ngawira mbele za mmeo haswa ukiwapa wadogo zako na ndugu za upande wako huku wa kwake ukiwapiga 'kibuti'? Kama ndiyo basi wewe ndiye tatizo na kama hapana basi kuna zaidi ambacho inabidi kueleweshana ili tuone pa kuanzia.
Tatu:
Una hakika ni mumeo tu au ni mume wenu? I mean, wewe ni mke wa ndoa halali ambapo una kila haki katika ndoa au mmeaminiana na kuamua kuanza kuishi pamoja? Kama hakuna ndoa baina yenu (inayotambuliwa na serikali) nitachemsha kwani huenda mwenzio ndo sasa kampata anayeona anamfaa kuwa mke... Hii inaweza kuwa habari mbaya kwako lakini bado si mwisho wa mahusiano yenu!
Nne:
Je washenga unaowaongelea ni watu wazima? Namaanisha ni watu wa makamo? Wakati anawasimulia ulitia neno? Wao walichukuliaje hali hiyo? Walitoa ushauri wa maana? Nini ulijifunza toka kwao?
Mara nyingi watu katika hali ya uchumba na wanapokaribia kuoana hukurupuka kutafuta washenga na kujikuta hawapati washenga sahihi na hivyo kubeba mamluki juu kwa juu na madhara yake mbeleni huwa makubwa. Aidha, matron na patron ni vema wawe watu wenye ndoa ili waweze kuwashauri kulingana na wao wanavyoyaishi maisha ya ndoa. Kama mlikosea na kutafuta wasela wataalam wa maneno tu hii inaweza kuwaathiri siku za usoni, washenga wakionekana si mali kitu msikimbilie kwa wazazi, kutana na matron au patron wanaweza kusaidia kabla hamjafikia pabaya.
Mwisho:
Ninaamini una mengi ya ziada na nilichoandika hakijakutosheleza, natambua wazi kuwa kuna chanzo cha yote haya, hii inawezekana kuwa imechochewa na masuala yenu binafsi (chumbani) ambayo yamepelekea hasira za mmeo naye anajikuta anakuwa mbogo. Kuwa mpole kwa mmeo, onyesha kumjali katika kipindi hiki ambacho mmetofautiana kidogo, mwambie mmeo ni jinsi gani unampenda, mweleze ni namna gani uliumizwa na kitendo cha yeye kukosa imani na wewe juu ya kitabu chako cha benki, usimwonee aibu kwani huyo ni mmeo!
Jaribu kuwa muwazi kwake, mpe 'account details' za benki na mwombe kama anaweza kukupa zake pia. Usimfiche password (neno au namba ya siri) ya akaunti yako! Penda kutumia hela yako kwa matumizi ya nyumbani na mfahamishe mmeo pindi ufanyapo hivyo, hii itamfanya aelewe mchango wako katika umoja wenu.
Nasisitiza: Ndoa si kitu kibaya, ni jambo la heshima na kusambaratika kwake ni dhahma kubwa kwa wapendanao. Kukosea ni jambo la kawaida na kuombana radhi hurejesha penzi lililoingia kiza.
Nakutakia tafakuri njema!
wapendwa wana jf naombeni msaada wenu katika hili;
mimi nipo kwenye ndoa ni mwaka mmoja sasa lakini matatizo ndani ya hii ndoa hayaishi.mimi na mme wangu wote tunafanya kazi ila kuna mambo nashindwa kuyaelewa na ninabaki njia panda!
Mwezi uliopita nilikwenda likizo nyumbani cha ajabu wakati najiandaa kuondoka asubuhi mme wangu akaninyang'anya card yangu ya benki eti akifikiria nitakwenda kuwapa pesa nyumbani kwetu!
Kwa kweli tulibishana sana hadi nikafanikiwa kuondoka na card yangu ila alikasirika sana hadi akasema nikirudi nije na wazazi wangu eti hanitaki tena!
Nimeenda likizo nimerudi yakawa yameisha cha ajabu tukawa tumetoka out na waliokuwa washenga wetu wa harusi acha aanze kusimulia yaliyotokea!
Mimi ninaamini katika kusamehe na kusahau lakini mwenzangu ukifanya kosa anakumbushia na makosa yaliyopita nashindwa kuelewa ni kwa nini?
Kwa kweli mimi inaniuma sana na kuna kipindi najiuliza hivi kweli huyu mme wangu ananipenda kweli?
Naombeni mnisaidie katika hili kutokana na hizi tabia za mme wangu mimi nifanye nini?
Amelie!
Kwakweli Invisible no doubt na bora uendeleee kuwa invisible mkuu,wewe lazima uwe qualified counsellor ila ndio safi.
I hope dada yetu atakua amepata auheni sana baada ya kupata maoni yako.
Nashukuru sana Invisible kwa ushauri wako!
Mimi ni Mkristo lakini si mkatoliki ni Mpentecoste hatukuwa na semina kabla ya ndoa ila mchungaji alitupa mawaidha siku ya ijumaa kabla ya ndoa!
Kwa kweli kuhusu mambo ya benki kila mmoja wetu anafahamu password ya mwenzake!Pia kuhusu simu hatuna mipaka yani akikuta simu yangu anaweza akaperuzi kama anavyotaka pia mimi nikiamua nachukua simu yake naiperuzi!pia kuhusu barua pepe kila mtu anapassiword ya mwenzake tuko huru kwa hilo halina tatizo!
mimi nikiwa na ngawira nasaidia pande zote mbili sibagui na wakati mwingine nasaidia ndungu wa mme wangu kuliko hata wangu!Nikisafiri nje ya Tz nikirudi naleta zawadi za pande zote ila mwenzangu akisafiri nje analeta za upande wa ndugu zake tu!
Ni mme wangu kabisa tulifunga ndoa kanisani kwa baraka zote za wazazi wa pande mbili na ilikuwa ni baada ya kufuata taratibu zote pamoja na kutoa mahali!
Washenga ninaowaongelea namaanisha Patron na Matroni ni wanandoa wameoana tangu 2004!
Patron na Matron walituambia wao wanavyoishi na walivyoelewana katika mambo yao ya kipato!sasa wao ni tofauti na sisi maana Matron ni mama wa nyumbani!wao Patroni akipata mshahara anaweka mezani then wanapanga na mke wake!Sisi kwa kweli mimi nikiwa na pesa huwa nanunua matumizi yote ya nyumbani!
Tatizo mme wangu alishanitamkia kuwa anataka anicontrol na mimi kwa kweli nilimjibu hataweza kunicontrol maana hata mimi nina haki zangu naomba uniambie labda nilikosea kumjibu kuwa hawezi kunicontrol!
mgiriki njooo uone hiii huku... mshana jr mambo hayo, MO11 njoo ukenue basiAmelie,
Rules for a Happy Marriage
- Never both be angry at the same time.
- Never yell at each other unless the house is on fire.
- If one of your has to win an argument, let it be your mate.
- If you have to criticize, do it lovingly.
- Never bring up mistakes of the past.
- Neglect the whole world rather than each other.
- Never go to sleep with an argument unsettled.
- At least once every day try to say one kind or complimentary thing to your life's partner.
- When you have done something wrong, be ready to admit it and ask for forgiveness.
- It takes two to make a quarrel, and the one in the wrong is the one who does the most talking.
Ukipata nafasi zisome hizo rules mara mbili kila week, zinafanya kazi vizuri sana. Ukisoma comment za watu hapo juu zina-appy kwenye hizo rules. Try them out
mbona mambo ya kuchepuka hajaweka
mimi sijui njia panda gani yupo sasa?
ya kwenda tanga au moshi ati
huko huko nadhani
eti manka ungekua wewe ungefanyaa ungefanyaje aisee....
ningekupenyua makalio