Ngoja niwe muwazi hapa kusema kweli baada ya kuoana nikawa mvivu sana natoka kwenye shughuli za kutafuta mkate wa kila siku nakuwa nimechoka kweli akiniomba "mchezo"kweli nikawa namnyima namwambia nimechoka!
Ila hili limekwisha baada ya kuhudhuria semina ya wanandoa iliyofanyika kwa Gamanywa kweli ilinisaidia ni nilimuomba MUNGU anitie nguvu ili nisimnyime mwenzangu!
Hehehe, yani hapa dadangu ndipo ulikoroga mambo! Nakusihi sana, ulimzoesha kumpa 'haki' yake na sasa gharama yake ndiyo hii.
Yote uliyodhania yanaanzia HAPA! Ni vema ukae chini naye, mwambie hivi:
"Mume wangu nakupenda sana, natambua kuwa unanipenda pia na hilo linathibitika kwa yote ufanyayo kwangu mkeo. Najua nakukosea sana mume wangu kwa kutokuridhisha kipindi unapohitaji hivyo, naomba unielewe kuwa si mapenzi yangu na naelemewa na kazi lakini bado nakuhitaji sana. Nitajitahidi kupunguza kazi zangu na kupangilia namna ya kuzifanya kwa mpangilio mzuri ili nipate fursa ya kuilinda ndoa yangu.
Sipendi hali inakoelekea lakini naomba unipe ushauri wewe juu ya nini nifanye."
Hapo mpe fursa yeye kuona anasemaje, msikilize kwa karibu sana ili uweze kutambua nini anafikiria. Bibie katika mapenzi/ndoa ni muhimu sana kutenganisha muda wa kazi na mahaba kwa mwenzio. Wengi hujilaumu kwa kosa la namna hii. Ndoa nyingi zimevunjika kwa u-bize wa wanandoa na wengi hujikuta wakijutia kukuta wanandoa wenzao wakiamua kwenda nje ya ndoa/mapenzi kusaka kile wanachodhani wanakosa.
Aidha mwenzio anadhani umemchoka, nakushaurini fanya kuwa na mpangilio wa kushirikiana kimwili walau mara 3 kwa wiki na ikishindikana kabisa basi mara 2. Itapendeza sana mkiwa mnabadili mazingira ya kufanya hivyo (isiwe nyumbani tu) ili kupata ladha ya kufanya tendo hili takatifu mkiwa maeneo tofauti tofauti. Usisubiri mmeo akutoe 'auti' bali kwakuwa inaonesha nyote mna kipato wewe pangilia vema ratiba yako, andaa kila kitu nyumbani kuhakikisha usalama wa maskani kwenu, mpe taarifa ya mapema kabisa kwa kumwambia kuwa kuna siku ungependa kutoka naye 'auti' kisha hakikisha unaenda hoteli yenye hadhi ya kuitwa hoteli (japo mara mbili kwa mwaka).
Hii inaweza kuonekana kuwa ni kichekesho lakini imewasaidia wengi! Nimeijaribu hii na nimeshaona matunda yake kwa mwenzi wangu
🙂.
Kisha hakikisha unakuwa msafi, usafi ni kitu muhimu sana katika mapenzi/ndoa. Kumbuka kuwa huyu ndiye aliyekuona wewe bora kuliko wote! Amekuridhia na yuko tayari kufa nawe! Mpe kila unachodhani anastahili lakini kuwa makini usije mzoesha vibaya. Epuka kufanya kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu! Itakugharimu si duniani pekee hata siku ya Kiama.
Bibie ni hili tu tatizo kubwa ninaloliona kwako ambalo wanandoa wengi linawakabili. Si rahisi kutambua athari yake, mbaya zaidi ukikuta mwenzi wako ni mkimya na anaamua ku-'riakti' anavyodhani ni sawa. Jazba za ghafla, maamuzi yasiyotarajiwa na vitu kama hivyo hutokana na mwenzi mmojawapo kuacha ama kupunguza 'makasheshe'. Najaribu kupunguza ukali wa maneno lakini naamini kama mwanandoa unanielewa.
Kama ulikuwa msafi endelea kuwa msafi, kama ulikuwa ukirudi/mkirudi kutoka kazini LAZIMA kubusiana basi fanya kumbusu. Kama ilikuwa kawaida yenu kuambiana 'nakupenda mme/mke wangu' usiache kwani ataamini sasa humpendi ama umeshapata 'kifaa' kingine mbadala. Mfanye ajisikie mfalme naye atakufanya malkia! Kuna vijizawadi vingine ni vidogo na havina thamani kwako lakini kwake vitakuwa na thamani. Hakuna cha dawa wala uchawi, atanasika tu!
Bibie, nakuomba kukiwa na tatizo zaidi tushirikishe. Akionekana kutoelewa somo tafadhali rejea hapa na kutufahamisha nini tatizo nasi tutajitahidi kuiweka sawa ndoa yako.
Hili wala halihitaji mtu kuwa wa dini au mwenye imani sana.
Umesahau, hata elimu haina nafasi. Ni kama wote mnakuwa watoto vile!
Wengi wetu tunasahau kuwa nguzo kuu za mahusiano ni wakati wa uchumba na pale mambo muhimu yaainishwe kabla ya kuishi, badala yake uchumba huwa juu juu kupeana zawadi,ahadi na kusahau jukumu lililo mbele. Mambo muhimu kabisa ya kuwekana wazi ili yasilete matatizo ni Matumizi ya pesa, idadi ya watoto, misingi ya malezi, masuala ya extended families, nk. Na ni vyema wote yani mume na mke wajue kila jinsia ina mtazamo kwenye mambo mbalimbali na kila mmoja akubali tofauti za mwenzake.
Na hasa wanawake hujisahau na kuhamisha mapenzi yao yote kwa watoto wakisahau nani anastahili kuwa 'festi boni' wao.
Pili endelea kuwa mfano bora wa kuwapenda ndugu zake sana bila ubaguzi, na kama ni mtu wa kujifunza atajifunza kutoka kwako.
Well said! Usishauri tu... Hata wewe mkuu teh teh teh!
La muhimu zaidi mwombe Mungu akupe busara unapoongea na mumeo, usiongee ukisukumwa na superiority bali humbleness na hakika kwa busara utaweza kumuelewesha mambo mengi naye atajifunza na kama nafsi yake i wazi ataomba msamaha.
Good point!
Hujachelewa kuchukua hatua,ichuke sasa na utaishi na amani-ni mapema mno kuwafuata councelors ambao nao wameoana juzi tu. Good Luck.
Councelling ya online inakuwa rahisi kwake kwani identity yake inabaki kuwa siri yake! Muhimu apate ujumbe.
Tatizo la wanawake wenye elimu na kipato juu ni hili tu kuwa juu hawataki kujishusha kwa waume zao kila kukicha matatizo ndani ya nyumba.
Ndo maana mimi sitaki kabisa kuoa na wala sioi leo wala kesho haya matatizo nayaona sana kwa jamaa zangu...
Oa wewe! Usiogope elimu ya mwanamke. Usiparamie wanawake, tafuta mke. Wanawake ni wengi lakini wa kuwa mke ni mmoja naye akija huna ujanja huo wa Mwana-FA! It's the matter of time.
2- Kama mlionjana kabla ya Ndoa, ujue ndoa yenu itakuwa ktk mashaka throughout, otherwise mnatakiwa mtubu na msirudie makosa. Ubaya wa kuonjana kabla ya Ndoa, kuna uwezekano mkubwa wa kuenda Nje ya Ndoa baada ya Ndoa...
Mkuu Chuma, haya mambo kwa nyakati za sasa ni kama hayakwepeki tu. Asilimia 90 na zaidi ya wanandoa ambao wamefunga ndoa zao kuanzia miaka ya 90 wametembea pamoja kabla ya ndoa. Yani mtu akishapeleka posa na kumvalisha pete ya uchumba basi shughuli inakuwa kama ndio imepata baraka zote!
4- Ushauri wangu mambo ya email na simu jiweke mbali usije kuumia roho bure... Kila mmoja ajiweke mbali na mwenzake...believe ukiona email/sms ya ajabu ya mumeo au Mkeo....from that point utaanza kuwa na waswas na mwenzako...Kila mmoja amtrust mwenzake...
Hii inategemea na tabia zenu! Kama mnaaminiana na ni wakweli basi mke au mme hana haja ya kuficha Email wala sms. Yani kwangu huwa naona kawaida kabisa, labda issues za kikazi, issues za kibiashara hizo ndizo unatakiwa unamweleza ukweli mwenzako lakini hatakiwa kuwa na access ya kazi zako. Hii ni muhimu kikazi! Hata mwenza wangu anajua najihusisha na JF lakini hajui password yangu! Nilimwambia "Kumradhi, hilo siwezi!"