Nipo Moshi kikazi, mbona utitiri wa shule kila kona ninayopita?

mtoa mada yawezekana upo sahihi ktk kijiji nilichotokea mimi tuna sekondari mbili za kata na mbili za binafsi ndani ya kijiji na sio kata
 
huko ndiko yanapatikana mazishi ya ccm na huwa hawasikilozagi porojo wanachagua wapigakazi tu

hivi mkoa wa Kilimanjaro una wabunge wa ccm wangapi na upinzani wangapi? madiwani wa ccm wangapi na wa upinzani wangapi? hizi data nafikiri ndio zitatuonyesha kwamvba wanachagua ccm au upinzani.
 
Hawa jamaa ni noma aisee nilijaribu kufanya research nikagundua kuwa zile courses za sience UDSM, MUHIMBILI, BUGANDO, KCMC na zile COURSES ZA MAMBO YA FEDHA UTAKOMA wamejaa balaaa. Haya majamaa yanachangishana sana katika kusomesha

Safi sana!,kumbe Wachagga ni watu wa kuigwa na Makabila yote ya Tz.
 
Serikali hakuna walichopendelea.. Hapo unaona miaka ya 50's huko watu wanajenga barabara, vituo vya afya na shule wakati huo babu na baba yake ZZK wanawinda kima msituni..

Mwaka 1959, 1960 Wachagga wakawa wanadai Katiba Mpya ya Serikali ya Uchagga, wakati huo babu na baba yake ZZK hajui hata katiba ni kitu gani.. Harakati za Siasa Uchaggani hazikuanza leo..

Miaka ya 60 upto 70 tayari Umeme na Barabara nzuri, magari ya watu binafsi havikuwa ishu sana kule mgombani, maji safi ya kunywa kijijini kwangu yanatoka kwenye tap bila hata kulipia senti. Nyerere akaogopa hiyo maana tayari wakati huo wachagga walikuwa washakamata pesa nyingi. Akaleta Azimio la Arusha, watu wakafirisiwa, inauma sana, mimi wakati huo naambiwa babu yangu alikuwa analima Ngano West Kilimanjaro na Karatu huko, anaagiza mafuta kutoa Asia anafunga mzigo anaenda kufanya Biashara Zimbabwe na Namibia huko wakati huo babu yake ZZK wanajifungia ndani saa 12 jioni kuogopa Sokwe.. Aise bila Nyerere kuleta lile Azimio si ajabu Kaskazini tungeshakuwa na nchi yetu..

Sawa sawa kabisa Mkuu mimi nakumbuka Kijijini kwetu umeme ulifika 1972 na Mwaka 1975 tukawa na umeme nyumbani kwetu. Na nyumba za tofali na bati Moshi zimeanza kujengwa kwa wingi hata kuliko Dar.
 
Kweli moshi wamejitahidi penye ukweli tuseme,viva wachaga.turudi kwetu tunaosifia moshi je mnajua mikoa mingine haindelei sababu ya chuki,ubinafsi na kusaidiana?huo ndio ukweli.wachaga wanapendana Sana,wanainuana na kusaidiana pia maendeleo ya kwao ni kipaumbele,kazi iko mikoa flani ni majungu,fitna Tu zimewazidi.mf mkoa Mara wazaliwa wa huko wengi Wako poa upstairs lakini mkoa wao uko nyuma Sana mnadhani tatizo ni nini,hampendani,majungu na fitna vimekithiri.hakuna atakaetamani kusaidia nyumbani.hongereni wachaga niseme tu umoja wenu ndio unaowasaidia.
 
wachagga wanapenda pombe kuliko kitu chochote kile hawana lolote

Pombe hizo hizo ndizo zimewaletea maendeleo,Mchagga anatafuta hela ya kunywa na hela ya kufanyia maendeleo wakati nyie wengine mnatafuta hela ya pombe,kuvaa na ngoma tuu.
 
Na vile Rais ajae atatoka Kanda yenu,patakua ulaya
pigeni hatua zaidi huku mikoa mingine ikisinzia.kila la kheri.
 
Moshi vijijini mbunge ni Cyril Chami kutoka ccm hunaposema wachagga ni wapinzani Una maanisha nini ?kata zote za kibosho madiwan ni wa ccm :confused::confused:

we nae wa wapi? kubali yaishe tu maana hata elimu uliyopata ni ya mashaka na kudhihirisha bado bongo lala , muhamko, hunaposema..... haaa unaboa bana hata herufi kutumia hujui. Ndio wako mbele si uongo kule wamezaliwa wamekuta baadhi ya barabara lami, maji ya bomba yako tangu 50. Dawa ni kujipanga ili kuiga mazuri ukikazana kubisha utazidi kuchelewa.
 
Acha matusi karne hii unashangaa shule mbona kwa sasa shule za kata ni mikoa yote!

Kweli unachosha hujui tofauti ya shule na majengo wewe, hizi shule za kata kwa serikali ni kero tupu shule mchepuo wa sayansi haina maabara unaliringia? shule zinazoongoza kwa kufeli? Acha wivu kubali na ukitaka kupata hasira ya maendeleo nenda moshi mwezi wa 12 uone jinsi wanavyorejesha makusanyo ya mikoani makwao acha kulia lia hapa.
 
Kwakwel....wachaga hawaitaki ccm ....tangu zaman ndo maana kwao maendeleo yapo....sio lazima serekali iwajengee....binafsi nimefika Rombo kuna shule karibu kila kijiji...nyingine wamejenga gorofa kabisa...na ccm kwao ni sumu..nashangaaa....Iramba walivyo maskini..ila wanaipenda ccm

Iramba inapatikana mkoa gani mkuu nijuze?
 
Wachagga mimi na wajua ni waoga na wabinafsi sana na hawana chochote kuanzia akili mpaka mipango ya biashara sema kutokana na kubebena,wizi na ulozi na ukabila hawana chochote

Aliyekuzidi amekuzidi tu..mimi kwetu mtwara wakina mama vibarazani umbea wababa wanacheza bao, maendeleo yatakuja kweli?
 
Sogea sogea hadi machame,kuna kijiji kinaitwa NRONGA wananchi wanaweka lami wenyewe

Aisee nimesoma Nronga kule ni balaa hakuna nyumba ya udongo na zaziwla ng'ombe huko ni kama nyumba ya kuishi mtu maan limejengwa kwa matofali ya cement na na mlango wa grill kabisa yaan Chagga's tupo juuuuuuu
 
Mkuu ni majuzi kati hapa umepitishwa mpango mkakati kila kata kuwe na chuo cha ufundi VETA na kwa baadhi ya vijiji kazi imeshaanza,,,,,,na watia nia wote wa ubunge wanalijua hilo....wakati kuna mikoa na wilaya hivyo vyuo havipo....kubalini kataeni kuna jambo la kujifunza kwa hawa watu.....mnaoponda ni vyema mkaondoa pamba masikioni....

Aisee nilikuwa sijasikia hii.. Hii ni habari njema zaidi
 
Serikali hakuna walichopendelea.. Hapo unaona miaka ya 50's huko watu wanajenga barabara, vituo vya afya na shule wakati huo babu na baba yake ZZK wanawinda kima msituni..

Mwaka 1959, 1960 Wachagga wakawa wanadai Katiba Mpya ya Serikali ya Uchagga, wakati huo babu na baba yake ZZK hajui hata katiba ni kitu gani.. Harakati za Siasa Uchaggani hazikuanza leo..

Miaka ya 60 upto 70 tayari Umeme na Barabara nzuri, magari ya watu binafsi havikuwa ishu sana kule mgombani, maji safi ya kunywa kijijini kwangu yanatoka kwenye tap bila hata kulipia senti. Nyerere akaogopa hiyo maana tayari wakati huo wachagga walikuwa washakamata pesa nyingi. Akaleta Azimio la Arusha, watu wakafirisiwa, inauma sana, mimi wakati huo naambiwa babu yangu alikuwa analima Ngano West Kilimanjaro na Karatu huko, anaagiza mafuta kutoa Asia anafunga mzigo anaenda kufanya Biashara Zimbabwe na Namibia huko wakati huo babu yake ZZK wanajifungia ndani saa 12 jioni kuogopa Sokwe.. Aise bila Nyerere kuleta lile Azimio si ajabu Kaskazini tungeshakuwa na nchi yetu..
Ha ha haaa.... Ume mshambulia Zio vikali sana, ila cha kuongezea wakati sehemu nyingine za Tanzania zikilia na uhaba wa bidhaa za viwandani miaka ya 1980's watu wa Kilimanjaro walikuwa wanazipata kwa urahisi via magendo tokea Kenya, na kipindi hicho wengine wakikomaa kulima maindi na kuuza kilo Tsh. 55 kahawa kilo moja ilikuwa inauzwa Tsh 1000. Na Mungu akiwabariki wote wakavuna gunia 20 nadhani mkulima wa maindi atapata pesa kidogo saaana kuliko yule wa kahawa. Na cha ziada wengine wakifuata maji makilomita sisi tulikuwa tuna maji safi kwenye mifereji yetu iliyo chimbwa na babu zetu miaka ya 1890's.
 
Back
Top Bottom