Nipeni Ushauri mwanana

zamani mimi nilikuwa Yanga.Siku hizi nimeachana na ushabiki/upenzi wa timu,michosho tu.Na zile kamati zao za ufundi zinaniudhi kama nini,badala ya kucheza soka wamekazania sangoma!
ushabiki/upenzi umehamishia wapi? chini,lager...
 
wewe mjanja lakini si sana KARIBU KWA MIKONO MIWILI.Huoni hata jezi na hata hivyo huwaga man u huwa unaangalia burudani na si kushabikia(LAKINI INAMAANA SIMBA au MAN U WAKIFUNGWA UTAHAMA?)
 
Kwanza hongera kwa kutambua kuwa umekaa pasipo kufaa na panapokuumiza akili..Pili,pole kwa kuumizwa na timu ulizokuwa ukishabikia.

Ninachokushauri ni kwamba,uje upande wetu wa Simba "wazee wa kuvunja rekodi" na sisi tutakupokea kwa mikono minne(manake miwili haitoshi)..Na sharti walijua,ukishabikia Simba ni lazima ushabikie Man U "mashetani wekundu"..

Ukija Simba ndo uamuzi wa busara na siku zote utakuwa mtu wa furaha..
 
Usifanye hivyo hata kidogo na naomba uendelee na msimamo wa ushabiki wako, hata mimi pia ni Yanga damu, lakini najipa moyo kuwa huenda mambo yakabadilika na pia uzalendo wa kutoka moyoni hauwezi nibadili msimamo wangu wa kuipenda yana. ewe umesahau ule msemo usemao nymbani ni nyumbani hata kama kijijini, sasa unataka kukana nyumbani kwenu? mwanao akinyea kiganja chako utakikata au utasafisha then unasonga mbele. Mkuu kuwa na moyo wa uvumilivu na lazima ukubali kuna kushinda na kushindwa kaka
 
Tuletee NEWZ, na sio kutuuliza vitu visivyo na kichwa wala miguu. kama umekosa la kuwaambia wana JF nyamaza kimya.


Mimi ni mshabiki mkubwa wa Dar es salaam Young African ya Tanzania pamoja na Liverpool Fc ya England.Kutokana na mwenendo mzima wa timu ninazozishabikia naona upo umuhimu wa kutuliza mawazo kwa kuchagua kwa muda timu zingine zinazofanya vizuri katika mashindano mbalimbali kwani 'kama mtu anaweza kubadili dini itashindikanaje kubadili timu ya kushabikia japokwa msimu mmoja?!'
Kwa maoni yangu hapa TZ ningependa kwenda upande wa pili wa shilingi namaanisha Wekundu wa msimbazi Simba na England pia Man U.Bila ubishi hizi ndio timu ambazo zitanitoa presha na mlolongo/mgandamizo wa mawazo kila kukicha.
Sasa wadau nyinyi kwa maoni yenu mnaona imekaaje?
 
Kuhusu timu za bongo sina ushauri maana niliacha kushabikia toka kipindi kile yanga ilipokuwa inawaka.

Kuhusu za uingereza, kweli ulipotea nakushauri uje kwenye right direction. Man U ndio timu, ila sasa ukianza kuwa shabiki ni mvua na jua. Yaani mimi hata Man U ifungwe bado nitakujibu naipenda Man U, yaani ndio my love wa pili hana mpinzani ukija moyoni mwangu.

Kama moyo wako sio ngangari chagua timu zenye historia nfedu za ushindi angalau unakuwa na uhakika
 
Ziondaughter huyu anakuchokoza eti eeh? Chini anamaanisha nini afadhali angeacha lager tu. Si eti Zion dadangu?
Yani huyu inaonyesha hana dada kwao sio kosa lake.Na mie sijamuelewa hiyo chini hapo anamaanisha nini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom