Nipeni Ushauri mwanana

mtanzaniaraia

Member
Aug 17, 2009
37
1
Mimi ni mshabiki mkubwa wa Dar es salaam Young African ya Tanzania pamoja na Liverpool Fc ya England.Kutokana na mwenendo mzima wa timu ninazozishabikia naona upo umuhimu wa kutuliza mawazo kwa kuchagua kwa muda timu zingine zinazofanya vizuri katika mashindano mbalimbali kwani 'kama mtu anaweza kubadili dini itashindikanaje kubadili timu ya kushabikia japokwa msimu mmoja?!'
Kwa maoni yangu hapa TZ ningependa kwenda upande wa pili wa shilingi namaanisha Wekundu wa msimbazi Simba na England pia Man U.Bila ubishi hizi ndio timu ambazo zitanitoa presha na mlolongo/mgandamizo wa mawazo kila kukicha.
Sasa wadau nyinyi kwa maoni yenu mnaona imekaaje?
 
Angalia afya yako kwa kufanya mazoezi, kutafakari na kuinua uchumi wako na familia yako na taifa kwa ujumla. Vinginevyo kichwa kitakuwa cheupe kwa kufikiri ushabiki na bado mambo muhimu yanakuandama. Utapata stroke kwa kushindwa kuhimili presha za ushabiki. Hebu angalia hapo ulipo umefanikiwa kitu gani kwakuwa shabiki wa vijana wa Afrika???? Tafakari wapi utainua hali ya maisha yako na kudumu katika hiyo
 
Tubakie Yanga wote mambo Manji atarekebisha ila kwa UK njoo ChelseaFC
 
Ushauri wangu,acha kujipa pressure zisizo na maana okoa muda wako.Hicho kiwango ulichofika si entertainment tena ila unajitafutia maradhi.Acha ushabiki and control yourself vinginevyo utakufa bure siku si zako.Si umeshasikia watu waliokunywa sumu eti timu yao imefungwa? ndio unakuendea.Take care!
 
Ndugu yangu wewe si shabiki ni mpenzi ungekuwa shabiki kama mimi husingekuwa unaumia, shabiki yeye anafurahia mpira unavyochezwa wacheze manyema au yanga anayecheza vizuri ndiye anayeshabikia ukiona unaumia ujue umetoka kwenye ushabiki umeamia kwenye upenzi waulize ndugu zako wa bwawa la maini wanavyoumia
 
Karibu Msimbazi kwa moyo mkunjufu na kadi za uanachama unaweza pata hata leo.
Halafu sikujua binamu Masanilo ni mdau wa Yanga. Pole sana binamu ndio kupokezana vijiti uko, msimu uliopita tulikuwa sie, msimu huu nyie, ndio football
 
Karibu Msimbazi kwa moyo mkunjufu na kadi za uanachama unaweza pata hata leo.
Halafu sikujua binamu Masanilo ni mdau wa Yanga. Pole sana binamu ndio kupokezana vijiti uko, msimu uliopita tulikuwa sie, msimu huu nyie, ndio football

Hahaa Jangwani mazee ndo masikani kila siku jioni nipo pale napata kahawa na akina mzee Yusuf Mzimba na Kina George Mpondela....karibu sana tutauwa mnyama hivi karibuni! Umoja wa mataifa
 
Njoo Arsenal mkuu
Naam hili chama langu pia
Ni pazuri sana hata wakifungwa lakini unakuwa umeburudika na kandanda tamu lenye ladha ya kibrazil na kifaransa. Sio uko kwingine ni bufu bufu bufu bufu, raha ya kandanda hakuna kabisa. The Gunners all the time:D
 
ha ha ha bora uchague kabisa....unaweza kufa.....the lesbian/gay way..........ha ha ha ha........

Sidhani kama kuna mtu anapenda kufa.Hebu niambie ukweli wako kabisa kama huogopi kufa wewe? Kufa tutakufa lakini mhh,mwenzangu.Labda kama unazungumzia kifo cha aina nyingine,mie sijaelewa.
 
zamani mimi nilikuwa Yanga.Siku hizi nimeachana na ushabiki/upenzi wa timu,michosho tu.Na zile kamati zao za ufundi zinaniudhi kama nini,badala ya kucheza soka wamekazania sangoma!
 
Ushauri wangu,acha kujipa pressure zisizo na maana okoa muda wako.Hicho kiwango ulichofika si entertainment tena ila unajitafutia maradhi.Acha ushabiki and control yourself vinginevyo utakufa bure siku si zako.Si umeshasikia watu waliokunywa sumu eti timu yao imefungwa? ndio unakuendea.Take care!
Nashukuru sana kwa ushauri nasaha ulizonipatia,kwakweli pressure huwa inapanda sana ninapoona timu yangu ikifungwa tena kizembe,nitajitahidi kuachana na mambo hayo ya ushabiki nadhani nitafanikiwa.Ahsanteni sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom