Mimi naua Jpili nikimuona yuko na mwanaume hakika mwingine akinikosa mimi
Mwanaume mwingine Ni wewe maana ndo ulimpigia, ukamtumia nauli aje jumapili.
Kwa hiyo hutaona mwanaume mwingine zaidi yako.
Ushauri:
Nenda jumapili mpokee, mpeleke nyumbani kwako maisha yaendelee.
Inatosha yeye kuona kwamba ameingia Chaka, maana alidhani amepata kumbe kapatikana, hili atalojutia na kamwe katika maisha yake hatakuwa Tena tayari kutongozwa kwenye simu.
Inatosha pia wee kuona umeingia Chaka, maana ulifikiri mkeo hatongozeki, kimbe ni maharage ya mbeya maji moja.
Kwa kifupi nyote wawili Ni wasanii, we utasema ulimjaribu ili uone Kama Ni mgumu kwa wanaume, karhalika naye atakwambia alijua kabisa Kama Ni wewe, ila alitaka akujaribu kama nawe Ni mdhaifu wa kutuma pesa kwa michepuko na kuwahi stendi kuipokea na kulala nayo.
Basi utakapokwenda jumapili utakapomwona just naye pia kakuona, Basi furahianeni, kumbatianeni, bisianeni maana ninyi nyote wasanii,
Basi maisha yanaendelea namna hiyo , na ndivyo ndoa nyingi zinavyodumu, sema tu wanandoa
Wengi wamefundishwa kupambana wenyewe na changamoto zao pasipo kukimbilia kuomba ushauri nje, maana Kila mtu anachangamoto yake katika ndoa, mshukuru Mungu angalau ya kwako ndo waijua leo!!!!