Nipeni tofauti

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Nisaidieni maana kuna mgeni mmoja kanipiga swali nikakwama.

Tofauti ya "huzunika" na "sikitika"
 
Kama aliyekuuliza anajua kimombo mtofautishie kwa maneno TO BE SAD (kuhuzunika) na TO REGRET (sikitika).
Subject to confirmation by linguistics.
 
SIKITIKA ni kuwa na hali ya uzuni kwa jambo fulani,haswa hali ya simanzi.na katika jambo baya.Baada ya kusikitika kinachofuata ni kuhuzunika.it may be.
 
Kusikitika kunachukua muda mfupi zaidi kuisha kuliko kuhuzunika.
Mfano" Umeibiwa gari? OOOH Nasikitika sana"
"Nasikitika hatutaweza kukuajiri."
Lakini kama umefiwa "unahuzunika" na unachukua hata miezi kuhuzunika. Huzuni sanasana inaenda na msiba.
 
HUZUNI-ka: grief, sorrow, mourning, distress, dolour= Hii hufuata na machungu moyoni. Inachukua muda mrefu kumliwaza mwenye huzuni.
SIKITI(KO)-ka: Sadness, disappointment, regret = Kutokuwa na furaha; kutoridhishwa na hali au tabia, kujuta au kujutia.
Mifano:
- Kifo cha baba yake kilituhuzunisha sote. Hapa mfiwa na wengine huwa na huzuni.
- Inasikitisha kumwona jinsi anavyolewa hadi kuaibika. Pengine hata mlevi mwenyewe hana masikitiko juu ya matendo yake.
- Jana nilikupa pesa, leo unataka tena. Nasikitika, leo siwezi kukusaidia. Hapa inaonesha kuvunjika moyo zaidi kuliko kusikitika.
- Unasikitika nini? Ninasikitika gari nimenunua mwaka jana tayari imeanza matatizo.
 
Maneno yote yaani huzuni na sikitika yana maana sawa yaani hali ya kuwa na uchungu moyoni, majonzi au jitimai kwa kutokewa au kupatwa na jambo fulani. Tofauti ya maneno haya iko katika mazoea ya matumizi ambayo msingi wake ni unasibu wa lugha. Kwa mfano imezoeleka kusema nasikitika kukuarifu kuwa suala lako haliwezi kushughulikiwa.... au tumepokea kwa masikitikiko makubwa taarifa ya kifo cha ndugu yetu...., tuna huzuni ya kufiwa......, n.k.
 
Watu mnaambiwa mtoe maana nyie mnatafsiri kwa kiingereza hii ndio tabia gani sasa.Ina maana kiingereza mnaakifahamu zaidi ya kiswahili?Tuache ushamba.Huzunika ni kielezi ambacho shina lake ni huzuni,ni hali ya kuwa na majonzi baada ya kupata aidha taarifa mbaya au inayomgusa mtu.Sikitika ni hali ya kuonesha kuwa na kama wasiwasi na jambo lisilo zuri,kumhurumia mtu,kuonesha hali ya kumjali mtu.Nawasilisha
 
Back
Top Bottom