Nipeni tofauti ya maneno "mungu" na "Mungu"

Nipeni tofauti ya maneno "mungu" na "Mungu"

erikomba

New Member
Joined
Dec 6, 2013
Posts
3
Reaction score
2
Habari zenu?

Kulingana na ufahamu wa kila moja wenu, nipeni tofauti za maneno haya- "mungu" na "Mungu"
 
Mungu= Supreme God
mungu= chochote unachokiabudu inaweza kuwa bosi wako, mkeo, majini unayofuga au hata we mwenyewe unaweza kujifanya mungu kwa kutisha watu au familia yako
 
Mungu na mungu hayana tofauti ya kimaana zaid ya uandishi moja imeanza na herufi kubwa nyingne kubwa
 
Tofauti hapo mm naona ni ktk uandishi tu moja umeanza na herufi kubwa na nyingine herufi ndogo
 
tofauti ni uandishi tu. fikiria kama maneno yote yangeandikwa kwa herufi kubwa. Hata hivyo kuna tofauti kati ya mungu na miungu
 
Mm nipo tofauti na nyinyi kuna mwenyeenzi mungu na mungu hawa mungu au miungu wapo wengi sana,ila mwenyeenzi ni mmoja tu jina halina wingi.unapoomba tumia neno mwenyeenzi mungu basis kwa uwezo wake password itafunguka
 
habari zenu- kulingana na ufahamu wa kila moja wenu, nipeni tofauti za maneno haya- "mungu" na "Mungu"

Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako maana hatakuhesabia kuwa una hatia mtu alitajae jina lake bure.
 
majibu ya msingi yametolewa.
Kazi ni kwako kuyasoma na kuyaelewa.
 
habari zenu- kulingana na ufahamu wa kila moja wenu, nipeni tofauti za maneno haya- "mungu" na "Mungu"

Katika lugha ya kiswahili,kuna aina ya maneno inaitwa NOMINO.....nomino imegawanyika katika makundi au aina kuu nne....ya kwanza ni nomino za PEKEE, ya pili ni nomino za KAWAIDA, ya tatu ni nomino za jamii na ya nne ni nomino dhahania....sasa neno Mungu linaangukia katika aina ya kwanza yaani nomino za PEKEE na maneno yote ambayo ni nomino za pekee lazima yaanze na herufi kubwa hata pale yanapoanza katikati ya sentensi.....so huwezi kuandika nomino hii kwa kuanza na herufi ndogo yaani ‘mungu' badala yake lazima uandike kwa kuanza na herufi kubwa....Mungu.
 
Aiseeh...mbona mnazunguka sana,jibu ni kwamba neno la kwanza limeanza na herufi ndogo na neno la pili limeanza na herufi kubwa.
 
Katika lugha ya kiswahili,kuna aina ya maneno inaitwa NOMINO.....nomino imegawanyika katika makundi au aina kuu nne....ya kwanza ni nomino za PEKEE, ya pili ni nomino za KAWAIDA, ya tatu ni nomino za jamii na ya nne ni nomino dhahania....sasa neno Mungu linaangukia katika aina ya kwanza yaani nomino za PEKEE na maneno yote ambayo ni nomino za pekee lazima yaanze na herufi kubwa hata pale yanapoanza katikati ya sentensi.....so huwezi kuandika nomino hii kwa kuanza na herufi ndogo yaani ‘mungu' badala yake lazima uandike kwa kuanza na herufi kubwa....Mungu.

Huyu ndiye Great Thinker wengine *#-*/!:🙁)??*+#
 
Mungu ni mmoja na aliye toa maana KAma mfano mungu ni kitu unacho kiabudu wongo ,huwezi xema anayeabudu ng'ombe ni mungu wake no
 
Ni vyema kama mtu anaandika Mungu (muweza wa yote) akaanza na herufi kubwa yaani (M).
 
Mungu ni mmoja na aliye toa maana KAma mfano mungu ni kitu unacho kiabudu wongo ,huwezi xema anayeabudu ng'ombe ni mungu wake no

sidhani kama upo sahihi mkuu kwani hata kwenye kiingereza (God) means the (Almighty) ila (god) au wingi (gods) ambayo ni miungu kwa kiswahili hapo mtu ana maana ya miungu mingine ikiwemo hiyo ya ng'ombe.
Nikosolewe kama na mimi nimekosea.
 
Vip kwenye kutamka Kuna utofauti? Cha muhim ni imani yako Na matayarisho ya moyo
 
Back
Top Bottom