Nipeni tofauti ya maneno "mungu" na "Mungu"

Nipeni tofauti ya maneno "mungu" na "Mungu"

Mungu= Supreme God
mungu= chochote unachokiabudu inaweza kuwa bosi wako, mkeo, majini unayofuga au hata we mwenyewe unaweza kujifanya mungu kwa kutisha watu au familia yako

Mf mzuri ni mungu Kanye West
 
majina yote ya pekee na dhahania uanza kwa herufi kubwa. km unamaanisha Mungu aliye pekee na tunaayemwamin kwa kusikia s kwa kumuona (kudhani) bas utahusisha hyo yenye herufi kubwa...kinyume chake tumia hyo herufi ndogo
 
"Mungu" ni Mungu wa kweli(nomino ya pekee) na huanza kwa herufi kubwa, mungu ya herufi ndogo ni shetani,miungu au kile unachokiabudu kama vile mizimu. Watu huandika "Namshukuru mungu kwa kuniamsha salama" pasi na kujua kuwa mungu(herufi ndogo)ni shetani. Soma 2WAKORINTHO 4:4 na 2WAFALME 1:1-2 utaona tofauti zake.
 
Ukisema mwenyenzi mungu ndio sahihi,herufi kubwa na ndogo hazina tofauti ktk kutamka
 
Ukitamka kwa kunong'oneza neno mungu au ukitamka kwa kupayuka neno mungu kuna tofauti?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom