Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,921
- 4,681
Niposa safarini nchi jirani kibiashara na nimeshukia nyumbani kwa rafiki yangu. Nimepewa chumba changu na ninalala humo peke yangu. Cha kunishangaza kama wiki tatu zilizopita nimeamka asubuhi nikakuta kiatu ninachovaa cha mguu wa kushoto ile carpet ya kukanyagia ndani ya kiatu imegeuzwa ndani nje. Nikajiuliza maswali mengi bila kupata jibu. Mimi ni mkristo nisiyetishika na mauza uza ya kishirikina nilikipiga kiatu damu ya Yesu na kuondoa shaka lolote. Wiki mbili baadae nimekivaa kiatu kile na hapakuwa na dhara lolote. Ninachoshangaa ni kwamba juzi usiku kuamkia jana nimeamka asubuhi na kukuta kiatu kile kile cha mguu wa kushoto carpet lake la ndani limegeuzwa ndani nje. Nimejiuliza maswali mengi na sikupata jibu ila mimi kama mkristo thabiti nimetupilia mbali dhana zote zinazoaminiwa ktk uchawi na uganga. Msingi huu nimeujenga juu ya uthabiti wangu kwamba sikuwahi kumwamini mchawi wala kumpa usikivu wa namna yeyote ile na pia sikuwahi hata kushika wala kuamini katika hirizi ya namna yeyote ile.
Hebu wanye hekima wa Jf tushirikiane katika hili ni nani au nini kinageuza carpet ya kiatu changu usiku? Nia na dhumuni ni nini? Niko fiti mentally na physically na sijaruhusu kwa namna yeyote kujiathiri kisaikolojia.
Hebu wanye hekima wa Jf tushirikiane katika hili ni nani au nini kinageuza carpet ya kiatu changu usiku? Nia na dhumuni ni nini? Niko fiti mentally na physically na sijaruhusu kwa namna yeyote kujiathiri kisaikolojia.