NIPENI MAJIBU YA HESABU YANGU HIi

NIPENI MAJIBU YA HESABU YANGU HIi

4+2x(8-3)/2-1

MAGAZIJUTO: 4+2 x 5/2-1 = 6x5/2-1 = 30/1 = 30.

Jibu = 30.

duh....mkuu umekokotoa kwa confidence kabisa halafu na rule ya magazijuto umeweka bila hata kutumia kweli kuna tatizo kwenye upande wa hesabu kwa watanzania wengi......kweli div 5 lazima ichukue mkondo wake
 
4+2x(8-3)/2-1MAGAZIJUTO: 4+2 x 5/2-1 = 6x5/2-1 = 30/1 = 30.Jibu = 30.
ayaaaaah, ungekuwa karibu ningekukoa kwenzi kidogo.. umeenda vizuri kabisa lakin ukasahau formula yako..MAGAZIJUTO.Kwa nin umejumlisha 4+2 kabla ya 2x5/2? haya angalia vizuri sasa.....4+2x5/2-1 = 4+5-1 = 9-1 = 8 jawabu na pigia msitari
 
1462985_10151812952741997_1064562609_n.png

= 8 (if bodmas applies)
 
4+2x(8-3)/2-1

MAGAZIJUTO: 4+2 x 5/2-1 = 6x5/2-1 = 30/1 = 30.

Jibu = 30.

Nina mashaka na jibu lako.
Hii ni MAGAZIJUTO (Fungua MAbano, GAwanya, ZIdisha, JUmlisha, TOa)

Here we go.
4+2(8-3)/2-1

Fungua Mabano
4+2x5/2-1.........(8-3=5)

Gawanya
4+2x2.5-1........(5/2=2.5)

Zidisha
4+5-1..............(2.5x2=5)

Jumlisha
9-1..................(4+5=9)

Toa
9-1=8
Jibu ni 8
 
4+2x(8-3)/2-1

MAGAZIJUTO: 4+2 x 5/2-1 = 6x5/2-1 = 30/1 = 30.

Jibu = 30.
Umekosa.

Umeshasema magazijuto. Hapo kwenye red ndipo kosa lako lilipo. Ulitakiwa kuanza na hiyo kabla ya kujumlisha then kutoa.

Waliosema jibu ni 8 wanastahili alama ya VEMA sana.
 
mmenichekesha sana waungwana,
tafsiri yangu kwa hesabu hii:-

kumbe kanuni wanayoitumia chadema bungeni ni magazijuto ambayo ccm wanaifahamu pia, tatizo jinsi ya kukokotoa, ccm wanawahi kwenye kuzidisha na kujumlisha, halafu wao wajifungia kwenye mabanooooo!

hatimaye wakiwa bado ndani ya mabano wanatoa jibu "THELETHINI" yaani "NDIYOOOOO"
Ni mtizamo wangu tu bandugu.
 
Mkuu katika fomula ya MAGAZIJUTO hutakiwi kuruka stage hata moja hesabu ya kwenye mabano umeifanya vizuri lakini umerukia kuzidisha kabla ya kugawanya afu ndio ufate kuzidisha, kujumlisha na mwisho kutoa ukifanya hivyo lazima utapata jibu 8

2(8-3) ni namba moja, kwa hiyo 14 ndio jibu sahihi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom