Nipeni madini ya nchi yote.....

New2JF

Senior Member
Oct 25, 2011
123
27
''Nipeni madini ya nchi yote ya Tanzania, then mimi nitayatumia kuilisha nchi yangu na Tanzania yote kwa miaka yote''. Haya ni maneno ya Rais Kagame wa Rwanda akimuambia JK na serikali ya Tanzania.

Mwana JF unasemaje kuhusu kailu hii? Hii ina maana gani?
 
Hii ni MATUSI kwa JK. Ila tunatakiwa kutafakari kwa nini tunataabika hapa nyumbani wakati rasilimali tunazo? Kagame kama kweli amesema, basi ni aibu yetu sote kuwa tuna viongozi vipofu wasioona kuwa utajiri wetu unapotea bila kuwanufaisha watanzania.

Tukiona hatuwezi kutumia utajiri wetu basi Tumsikilize kagame...!
 
Maana yake ni kwamba anamwambia JK kuwa "Wewe JK ni mjinga, mnakuwaje masikini na mna utajiri wa kutosha wa madini"?
 
Kagame yuko kikazi zaidi - kutumikia waliomtuma na kuhakikisha wananchi wananufaika na resources zake ziwe natural or otherwise.
Anatushangaa kwa nini tu maskini na tuna njaa wakati tuna kila kitu (kumbuka utamu wa madini anaujua, alivamia DRC na kupora madini mengi tu) na nchi yake inategemea kahawa tu lakini uchumi wake ni afadhali kulinganisha na wa kwetu. Hapo hajahitaji mbuga z
a wanyama.
Cha kushangaza hawa watawala wetu wala hawapatwi na wivu wa kuendelea, maadamu wao kila kitu ni serikali inalipia.
 
Kagame is right na JK nadhani atakuwa alihisi katukanwa maan wakwere wakipewa live huwa wanamind kama yule paroko alivyowananga live kuwa wako bize na ngoma tuu kusoma na kufanya kazi kwao mwiko
 
''Nipeni madini ya nchi yote ya Tanzania, then mimi nitayatumia kuilisha nchi yangu na Tanzania yote kwa miaka yote''. Haya ni maneno ya Rais Kagame wa Rwanda akimuambia JK na serikali ya Tanzania.

Mwana JF unasemaje kuhusu kailu hii? Hii ina maana gani?

tupe kwanza chanzo cha habari ili tukianza kutokwa na mapovu kama kawaida yetu hapa jf basi tuwe na mahali pa kuegemea!!
 
Mbona mnapenda kurudia rudia jambo.

Kwani mkuu alipokuwa Davos, aliambiwa nini na minjemba ya majuu?

Kauli inajieleza kwa umakini. Jamaa hajaimudu nchi. Lakini anafanya maksudi. Si alichaguliwa na 27% ya wapiga kura. Kwa vile mlimsaliti basi naye anafayizia woooooote.
 
Back
Top Bottom