Nipeni dakika chache(wanaume na wanawake)

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
16,920
Reaction score
28,497
Mara nyingi safari yetu hapa duniani (njiani) huwa ni fupi sana, ndiyo ni fupi ila cha ajabu tunadhani kwako itakuwa ndefu kwa kuwa tuu una pesa, mtu wa heshima yake, una mamlaka! Yale ya kuwaatiisha wengine nao wakatii!
Lakini tunasahau sisi safari yetu ni moja! Mkubwa kwa mdogo, mnene kwa mwembamba, mweusi kwa mweupe!

Nilipokuwa mdogo nilidhani wenye pesa hawapo kwenye safari tuliopo sisi,, wenye mamlaka hawapo kwenye safari yetu sisi, wazuri na warembo hawapo kwenye safari yetu sisi!

Kumbe nilikosea sana.
Wakati wewe tunapokushusha kwenye shimo futi kadhaa kwenda chini, hautasikia, hautawaona wale wapambe wako, wenye kuvaa suti maridadi, hautamuona yule kipenzi chako!
Zaidi tutakuwepo sisi wanyonge tukiomboleza kuondokewa nawe mpendwa wetu,
Wewe mpendwa wetu ulietufanya wanyonge tutii amri bila shuruti, nasi tukatii bila shida,.
Lakini sasa uko kwenye safari ambayo ulidhani ni ya kwetu sisi wanyonge tuu!.

Nilizaliwa nikiwa uchi, nami nitarudi nikiwa hivyo!
Sioni sababu za mbwembwe hizi za kidunia wakati safari yetu ni moja!
Maringo ya nini Mimi Pancho??
Nina pesa sana? Ni handsome sana? Msafi sana?? Hapana mwisho wa yote nakuja kugundua kuwa safari yetu ni moja navitupa vyote hivyo kando, badala yake nampa heshima inayostahili Msafiri mwenzangu, mwenzangu ambaye tupo ndani ya safari moja! haijalishi awe nani!

Baada ya hapo tutarudi nyumbani kwako na kufungua maturubai ndipo utakapojua mkubwa ni mmoja tuu

MUNGU pekee.

tutafakari

"Pancho boy
 
Yaani watu wanatishana tuu eti ishi vizuri na watu ..ishi bila maringo

Iko hivi ukishakufa wanaobaki duniani watu ndio watahuzunika , watununa , watajaza maneno ya chuki we zako umelala ..ata waamue kukuzika umesimama

Kifo alifichiwa kila mtu .... ata hao wanyonge wakilia hatowaona si ni sawa tu
 
Sawa mkuu asante sana
 
Mara nyingi safari yetu hapa duniani (njiani) huwa ni fupi sana, ndiyo ni fupi ila cha ajabu tunadhani kwako itakuwa ndefu kwa kuwa tuu una pesa, mtu wa heshima yake, una mamlaka! Yale ya kuwaatiisha wengine nao wakatii!
Lakini tunasahau sisi safari yetu ni moja! Mkubwa kwa mdogo, mnene kwa mwembamba, mweusi kwa mweupe!

Nilipokuwa mdogo nilidhani wenye pesa hawapo kwenye safari tuliopo sisi,, wenye mamlaka hawapo kwenye safari yetu sisi, wazuri na warembo hawapo kwenye safari yetu sisi!

Kumbe nilikosea sana.
Wakati wewe tunapokushusha kwenye shimo futi kadhaa kwenda chini, hautasikia, hautawaona wale wapambe wako, wenye kuvaa suti maridadi, hautamuona yule kipenzi chako!
Zaidi tutakuwepo sisi wanyonge tukiomboleza kuondokewa nawe mpendwa wetu,
Wewe mpendwa wetu ulietufanya wanyonge tutii amri bila shuruti, nasi tukatii bila shida,.
Lakini sasa uko kwenye safari ambayo ulidhani ni ya kwetu sisi wanyonge tuu!.

Nilizaliwa nikiwa uchi, nami nitarudi nikiwa hivyo!
Sioni sababu za mbwembwe hizi za kidunia wakati safari yetu ni moja!
Maringo ya nini Mimi Pancho??
Nina pesa sana? Ni handsome sana? Msafi sana?? Hapana mwisho wa yote nakuja kugundua kuwa safari yetu ni moja navitupa vyote hivyo kando, badala yake nampa heshima inayostahili Msafiri mwenzangu, mwenzangu ambaye tupo ndani ya safari moja! haijalishi awe nani!

Baada ya hapo tutarudi nyumbani kwako na kufungua maturubai ndipo utakapojua mkubwa ni mmoja tuu

MUNGU pekee.

tutafakari

"Pancho boy
Pancho boe
 
Maelezo mengi sana ila maana ni moja! hata ingekuwa umeandika kwa kifupi mbona ungeeleweka tu.
 
Back
Top Bottom