Nipate wapi kitabu kizuri cha ujasiriamali hapa Mwanza?

gikaro

Member
Oct 20, 2018
21
7
Ninauliza wakuu,

nisaidie ili nijue sehemu wanakouza vitabu vya ujasiriamali namna ya kufanikiwa. Niko hapa Mwanza na kama unajua bei yake nambie nitashukuru endapo wadau watanisaidia kujua hili jambo.
 
Mkuu mimi nakupa ushauri kutokana na uzoefu wangu. Ujasiriamali hausomwi kutoka kwenye vitabu. Ndiyo kusoma kunaongeza maarifa lakini kwa hizi nchi zetu za Afrika ujasiriamali mzuri ni ule wa kujifunza kutoka mitaani.
 
Unapoongea na jamii ya Tanzania usitumie maneno haya

1)Vitabu vya ujasiliamari badala ya motivational books.

2)Nataka utajiri badala ya Nataka mafanikio.

Ukiandika nilivyoelekeza utapata majibu mazuri ila kama hivyo ulivyoandika utapoke negatives tu.
 
mkuu achana na vitabu ingia mtaani ujifunze vizuri...mimi toka nipo sekondari nasoma vitabu vya ujasiriamali sijui akina Robert kiyosaki.

majuzi hivi nimeingia mtaani kuapply nilichosoma, .

aisee mambo ni tofauti kabisa
 
Unazani ktabu kitakupa mtaji na mbinu za ujasiriamali
Mkuu mimi nakupa ushauri kutokana na uzoefu wangu. Ujasiriamali hausomwi kutoka kwenye vitabu. Ndiyo kusoma kunaongeza maarifa lakini kwa hizi nchi zetu za Afrika ujasiriamali mzuri ni ule wa kujifunza kutoka mitaani.
Kwa nini ujasiriamali hausomwi kutoka kwenye vitabu? Unasema ujasiriamali mzuri ni ule wa kujifunza kutoka mitaani, kwani hicho kilichoko mtaani hakiwezi kuandikwa kwenye kitabu na mtu akajifunza kwa kusoma kitabu hicho?
 
mkuu achana na vitabu ingia mtaani ujifunze vizuri...mimi toka nipo sekondari nasoma vitabu vya ujasiriamali sijui akina Robert kiyosaki.

majuzi hivi nimeingia mtaani kuapply nilichosoma, .

aisee mambo ni tofauti kabisa
milionea wa kesho, unaweza kutoa mfano wa ulichosoma kwa sijui akina Robert kiyosaki na ulipoenda mtaani kuapply ukakuta mambo ni tofauti kabisa? Kama hautojali kujadili!
 
Kwa nini ujasiriamali hausomwi kutoka kwenye vitabu? Unasema ujasiriamali mzuri ni ule wa kujifunza kutoka mitaani, kwani hicho kilichoko mtaani hakiwezi kuandikwa kwenye kitabu na mtu akajifunza kwa kusoma kitabu hicho?
Theory na practicle ni vitu viwili tofauti. Kusoma sikatai kwani hata mimi ni mpenzi wa kusoma sana, ila ''ukisoma'' kwa macho kutoka kwenye kitabu cha ''mitaani'' unapata knowledge nzuri zaidi.
 
Theory na practicle ni vitu viwili tofauti. Kusoma sikatai kwani hata mimi ni mpenzi wa kusoma sana, ila ''ukisoma'' kwa macho kutoka kwenye kitabu cha ''mitaani'' unapata knowledge nzuri zaidi.
Ok, labda unaamaanisha kupractice unachosoma? Kwa sababu, ili upractice(kufanya kwa vitendo) ni lazima uwe na wazo au ufahamu(knowledge), Huu ufahamu unaupataje ili ukautumie huko mitaani, huu ujasiriamali unaosema unaupata mtaani unaupatapataje? (Muda mwingine uwasilishaji ni mgumu, naomba unielewe kwamba sikubishii unachosema, ila nahitaji ufafanuzi zaidi)
 
Mleta mada, vitabu viko kibao, na mimi nakushauri soma, sana tu sana, kama unajua kimombo soma THE RICHEST MAN IN BABYLON.

Lakini kusoma tu haina maana, cha muhimu ni kutekeleza ulichokisoma.

Inasemekana kwamba, ukiwa unafahamu kusoma lakini hausomi, uko sawa tu na yule ambae hajui kusoma kabisa, na mimi nasema hivi, ukisoma maarifa mazuri halafu ukashindwa kuyafanyia kazi, hauna tofauti na yule ambae hakuyasoma maarifa hayo.
 
Asante sana wana jamii forum maoni yenu ni mazuri zaidi na nimeishaanza kuyafanyia kazi , samahn kwa wale ambao tulishindwa kuelewana ,
 
Ninauliza wakuu,

nisaidie ili nijue sehemu wanakouza vitabu vya ujasiriamali namna ya kufanikiwa. Niko hapa Mwanza na kama unajua bei yake nambie nitashukuru endapo wadau watanisaidia kujua hili jambo.
Unaweza kwenda sido mwanza
KUna ofisi wanafundisha utengenzaji wa abuni za maji,miche na batiki pia kama uko interested
 
Back
Top Bottom