Nipake rangi gani ambayo itaweza kuendana na mabati ya GSM na ambayo hayatababuka?

Naikuru

Senior Member
Jul 29, 2015
167
226
Wakuu habari za wakati huu.

Nimelazimika kuingia humu kuomba ushauri kwa ajili ya kapata namna kumpa mke wangu amani ya moyo.

Nina mshukuru Mungu tumejenga nyumba kubwa nzuri na kufanikiwa kupaua kwa mabati ya GSM yale yasiyo ya rangi, huwa ni alluminium tupu.

Majirani zetu nao wamejenga nyumba zao nzuri kwa mabati ya rangi tofauti tofauti ili mradi tu kila mtu nyumba yake iwe kivutio kwa kila apitaye jirani macho yake yaelekee kwenye mapaa yao Jambo ambalo Mimi sikuzingatia.

Kilichonileta humu ni mke wangu hana amani kabisa na hili paa letu, anatamani lipate rangi lifanane na majirani wakati huo uwezo wa kusema ninunue bati 192 ya rangi ili tubadilshe kwa kweli sina na wala mpango hapo. Nimeona maeneo fulani watu wanapaka paa rangi ila baada ya muda rangi zinababuka na paa kuwa mbaya zaidi na bora ingebaki hivyo hivyo. Sasa mke wangu hana amani anataka tupake rangi paa letu.

Ombi langu wanajamvi nipake rangi gani ambayo itaweza kuendana na mabati ya GSM na ambayo hayata babuka?
 
Nenda maduka ya rangi, kaulizie roof paint na pia watake ushauri, rangi gani uichukuwe ambayo haita babua bati kwa muda mfupi
 
Kwanza mshukuru Mungu kwa kufanikiwa kujenga.

Pili huwezi mridhisha mke 100% mweleweshe kistaarabu kuwa uwezo wenu ndipo ulipoishia . Kupaka rangi nikuharibu ulichochagua kwa uwezo wako.

Nashauri mipango iwe kujenga nyingine mtakakayoezekea bati ya rangi tena ya ALAF
 
Kwanza mshukuru mungu kwa kufanikiwa kujenga.
Pili huwezi mridhisha mke 100% mweleweshe kistaarabu kuwa uwezo wenu ndipo ulipoishia . kupaka rangi nikuharibu ulichochagua kwa uwezo wako.
Nashauri mipango iwe kujenga nyingine mtakakayoezekea bati ya rangi tena ya ALAF
Natamani nikufanye rafiki unafaa
 
Kilichonileta humu ni mke wangu hana amani kabisa na hili paa letu, anatamani lipate rangi lifanane na majirani wakati huo uwezo wa kusema ninunue bati 192 ya rangi ili tubadilshe kwa kweli sina na wala mpango hapo
Mkuu, hebu ongea na mke wako vizuri illi uelewe haswa shida yake ni nini? Isije kua ni zaidi ya rangi ya Paa; Usije ukamaliza hilo ukaambiwa madirisha yawe kama ya XXX, pavement iwe kama ya wale pale n.k.
# Hongera kwa ujenzi
 
yawezekana kuna shida mahali
 
Jengeni nyingine mweke mabati ya rangi. Acheni kuumiza kichwa kwa kitu ambacho hakiongezi thamni. OVA Kama akiendelea kukosa amani mwambia talaka itamhusu.
 
Mwanamke ni Kiumbe wa ajabu Sana na ni ngumu Kumridhisha Siku zote Kwani Kama Mungu tu alishindwa mkamilisha na "anakosolewa" hadi leo je, wewe utaweza?

Fikiria KE Kaumbwa vizuri lakini;
1. Ana vaa wigi..
2. Anajichubua awe "mzungu"
3. Kucha, anaunganisha awe "jini"
4. Nk nk
So, please you are the head of the family. Be a Man !
 
Sorry mdau

Hivi dhana ya kwamba majini wana kucha ndefu niyakuthibitika?
 
Wakuu habari za wakati huu.

Nimelazimika kuingia humu kuomba ushauri kwa ajili ya kapata namna kumpa mke wangu amani ya moyo.

Nina mshukuru Mungu tumejenga nyumba kubwa nzuri na kufanikiwa kupaua kwa mbati ya GSM yale yasiyo ya rangi, huwa ni alluminium tupu.

Majirani zetu nao wamejenga nyumba zao nzuri kwa mabati ya rangi tofauti tofauti ili mradi tu kila mtu nyumba yake iwe kivutio kwa kila apitaye jirani macho yake yaelekee kwenye mapaa yao Jambo ambalo Mimi sikuzingatia.

Kilichonileta humu ni mke wangu hana amani kabisa na hili paa letu, anatamani lipate rangi lifanane na majirani wakati huo uwezo wa kusema ninunue bati 192 ya rangi ili tubadilshe kwa kweli sina na wala mpango hapo. Nimeona maeneo fulani watu wanapaka paa rangi ila baada ya muda rangi zinababuka na paa kuwa mbaya zaidi na bora ingebaki hivyo hivyo. Sasa mke wangu hana amani anataka tupake rangi paa letu.

Ombi langu wanajamvi nipake rangi gani ambayo itaweza kuendana na mabati ya GSM na ambayo hayata babuka?
Nenda kwenye hardware store waambie wakupe rangi ya bati PVA ya chaguo lako.
 
Acha

Acha uboya, utashikiwaje akili na mwanamke. Paka rangi aidha PVA roof -colour:Brick Red au Red au rangi yoyote mkeo anayoipenda ya kampuni ya Plascon zamani Sadolin. Ila bati liwe limekaa kwenye jua angalau miaka miwili toka uliezeke
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom