MSAADA: Mabati ya 'reject' yamekufikisha wapi baada ya muda gani?

mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
923
1,586
Salaam wakuu,

Ninataka niezeke kwa mabati yanayofahamika kama reject, nimetembelea wanapouza nimeona ni mapya kabisa hayana tofauti kubwa na yale ya madukani ambayo siyo reject.

Kuna mtu ameshawahi kuyatumia haya mabati au anafahamu mtu aliyewahi kuyatumia na hali yake ikoje mpaka sasa kwenye paa na yakadumu kwa muda gani? Ama ninunue nipake rangi? Nimepiga hesabu nimeona nitaokoa 500 000 nzima nikiezekea hayo.

Ninafuatilia comments zenu.
 
Kuwa makini sana. Mimi nilijenga banda la kuku likiwa na plan B ya kupangisha mradi ukizingua. Ndani ya siku 0 nyumba ilikuwa inavuja kama mwembe. Achana nayo
Inaonekana wanavyo ya classify kuwa REJECT kuna mashine wanatumia kutambua udhaifu na matundu yasiyoonekana kwa macho. Hata hivyo nilivyouziwa ni bora ningenunua dukani kwa jumla kwani bei ni karibu ile ile kama hujui kupatana kama mimi. Wale wauzaji wanaangalia umekujaje? Halafu wanakupa BEI
 
Shukrani sana
 
Haya haya ya dukani yanayoitwa msauzi asilimia kubwa ni reject kwani nlishashuhudia pale Tegeta yakiwa plain kabisa na yakapangwa rangi na muuzaji na kuwa mapya kabisa, unaweza sema kachukua alaf kumbe ushapigwa ukiweka muda mfupi 2 yanapauka na kulika na kutu.
 
Haya haya ya dukani yanayoitwa msauzi asilimia kubwa ni reject kwani nlishashuhudia pale tegeta yakiwa plain kabisa na yakapangwa rangi na muuzaji na kuwa mapya kabisa unawaeza sema kachukua alaf kumbe ushapigwa ukiweka muda mfupu 2 yanapauka na kulika na kutu.
Suala la uaminifu tumeachwa mbali sana sisi huku TZ. Nilienda sehemu huko majuu jamaa ni waaminifu sana wakikuambia kitu kipo sawa amini. Huku Duh! hadi Supermarket wakiweka SALE say 75% ya original price usipokuwa makini unauziwa bei ya awali. Ukistuka ndo wanakwambia tulikuwa hatujabadili bei.
 
Mfano mzuri tu nenda sehemu wanapouza mbao, waambie naomba nitumie tepu yangu staki ya kwenu utaona wanavyojiuma. Kwakweli uaminifu hapa Tanzania una approximate 0 kwani hizo tepu nazo zinachakachuliwa sana na ukirudi ktk mabati ndo kabisa unapigwa K O raundi ya kwanza 2
 
Ile nafuu ndio yenye ghalama Ni vyema uwatafute makampuni ya mabati kwenye website zao ufanye kulinganisha wapi unakoweza kununua Kisha ufanye maamuzi, kampuni za mabati Ni nyingi kuanzia alaf,waja,dragon, bati Bomba na nyingine nyingi na utofauti wa bidhaa zao sio mkubwa
 
Back
Top Bottom