Nionyesheni mradi wowote wa Samia 2021-2025

Nionyesheni mradi wowote wa Samia 2021-2025

Nionyesheni mradi wowote wa Samia wenye multiple effect angalau wa trion 1 alioanzisha Samia katika utawala wake pamoja na kukopa trion 50 ndani ya miaka 4!!

Huo mradi nikiuona najiunga ccm
Kila siku zinawekwa nyuzi humu za mengi anayoyafanya, busara sahihi ni kuzitembelea na kujionea.
 
Kila siku zinawekwa nyuzi humu za mengi anayoyafanya, busara sahihi ni kuzitembelea na kujionea.
Wakumbushe angalau miradi miwili aliyoianzisha mama samia ili waache midomo, angalau wewe unaweza kueleza in detail kwamba mradi huu,na huu ameanzisha mama na imefikia hatua hii! Mbona rahisi tu? Mbona ya magufuli ilikuwa wazi kabisa licha ya yeye pia kulazimika kukamilisha miradi ambayo iliachwa na mtangulizi wake?
 
Nionyesheni mradi wowote wa Samia wenye multiple effect angalau wa trion 1 alioanzisha Samia katika utawala wake pamoja na kukopa trion 50 ndani ya miaka 4!!

Huo mradi nikiuona najiunga ccm
Mradi wa chawa fc, baiskeli za samia, ...royootuaaaa,
 

Attachments

  • Duh kiongozi kama huyu mchapa kazi kumpata tena ni mitano tena 🫣.mp4
    947.9 KB
Wakumbushe angalau miradi miwili aliyoianzisha mama samia ili waache midomo, angalau wewe unaweza kueleza in detail kwamba mradi huu,na huu ameanzisha mama na imefikia hatua hii! Mbona rahisi tu? Mbona ya magufuli ilikuwa wazi kabisa licha ya yeye pia kulazimika kukamilisha miradi ambayo iliachwa na mtangulizi wake?
Samia hakutakiwa kuanzisha mradi mkubwa kabla ile mikubwa ya JPM haijaisha, SGR inakaribia kuisha. Daraja la Busisi limeisha. Ndege JPM aliziacha 12 zinanunuliwa tatu na Samia.

JPM aliacha viwanja vingi vya ndege vikiwa vinaendelea kujengwa, karibu vyote SSH kavimaliza.

Yapo mengi yanayofanyika muda huu. Samia alichoweza ni kurudisha imani ya wafanyabiashara waliokuwa wakiporwa pesa zao na hayati JPM mpaka ikafika wakati wakakimbilia nje ya nchi.
 
Kabisa yani huyu mama tunamchukulia poa tu lakini hipo siku tutaelewa
1:Miradi yote amepokea ikiwa 20-30,lakini amesha maliza
2:Kajenga shule za sekondari za sayansi kama 26 kwa ajili ya wasichana
3: vifaa vya CT scan,MRI ambayo vilikuwa changamoto amesambaza
4: Hospital now,vituo vya afya vimejazana
5:Vyuo vya Veta
6:Miradi ya maji
Nk
Tunasumbuliwa na upuuzi wa mfumo dume, jinsia yake inahukumiwa kuliko kile anachokifanya.

Samia atafanya mema tisa na baya moja lile baya litachukua nafasi ya yale mema tisa.
 
Nionyesheni mradi wowote wa Samia wenye multiple effect angalau wa trion 1 alioanzisha Samia katika utawala wake pamoja na kukopa trion 50 ndani ya miaka 4!!

Huo mradi nikiuona najiunga ccm
Ulitaka miradi iliyoanzishwa kwenye awamu ya 5 itelekezwe ili aanzishe mingine? Hujui kuwa alikuwa makamu wa Rais kwenye awamu ya 5? Kuna watu mna makamasi vichwani badala ya ubongo.
 
ndugu usichukulie pupa kwanza ungekaa ukafikiria kwanza kabla ya kuja kuandika uharo wako hapa, iko hivi, wakato mtangulizi wake anatoka aliacha miradi mingi sana ya matrilioni ya pesa alichokifanya ni kuendeleza miradi hiyo kama unavyoona sasa daraja mwanza, bwawa la umeme vyote vimekamilika kwa ufanisi mkubwa chni ya mam SSH asingeweza kuanzisha miradi mipya wakati kuna iliyoanzishwa na ujue alikuwa anatekeleza ilani ya uchaguzi hivyo punguza chuki kwa mama MITANO TENA
umeisoma ilani ya uchaguzi kweli wew?!Au unajaribu tu kujibu.Anyways nikukumbushe kuwa kwenye ilani ccm ilisema kufikia 2025 umeme utakjwa kila kijiji Tz,ilisema maji safi na salama itakuwa 80% kwa vijijini na 100% maeneo ya mjini(vip ulipo kuna maji safi na salama)?,ilisema kila shule ya sekondari itakuwa na huduma ya internet na kompyuta za kujifunzia(vipi huko ulipo)?Hyo ilani yako inayosemea daraja la Busisi unaweza kunionyesha page?
 
Nionyesheni mradi wowote wa Samia wenye multiple effect angalau wa trion 1 alioanzisha Samia katika utawala wake pamoja na kukopa trion 50 ndani ya miaka 4!!

Huo mradi nikiuona najiunga ccm
Utambuzi wa Viongozi wa jadi na watemi
 
Hakuwahi kufanya chochote hELa zote wametoa walipa kodi pamoja na mikopo na misaada to ka kwa nchi wahisani

Na kwa taarifa yenu SGR ni mkopo mrefu sana toka kwa Exim Bank ya Singapore, na ni deni ambalo hatutaweza lilipa kamwe
 
Nionyesheni mradi wowote wa Samia wenye multiple effect angalau wa trion 1 alioanzisha Samia katika utawala wake pamoja na kukopa trion 50 ndani ya miaka 4!!

Huo mradi nikiuona najiunga ccm
Ilani ya CCM au ya Samia?
 
IMG-20250620-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom