NIONAVYO: Tulia Ackson kuwa Spika wa kwanza kushindwa kutetea kiti chake cha Ubunge

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Nimetafakari mambo mawili moja nini kilitokea uchaguzi uliopita na khali ya kisiasa ya sasa namwona Mhe. Tulia Ackson kudondoshwa ubunge na Msomi Boniface Mwabukusu.

Namwona Spika kuendelea kuwa spika hata baada ya kuanguka ubunge wa jimbo la uchaguzi wa Mbeya mjini kwa sababu ya mchango wake wa kupitisha Azimio la bunge la mkataba wa kuuza bandari zetu.

Hahitaji pia kiwa mbunge kuwa spika ingawaje baada ya kuanguka atakuwa kadhoofika kisiasa. Na pia nawaona sisiemu kumfyagilia Msomi Mwabukusu kwa kumfutia leseni yake ya uwakili na kumtajataja kila mahali.

Bila kujijua wanampigia bonge la kampeni ya kuwa mbunge.

Yule mwanamuziki wa kufokafoka najua anakinyemelea kiti lakini wapigakura wanataka damu mpya kwenye siasa za jimbo lao.

Hivyo, Sugu hatakuwa mbunge ataanguka kwenye kura za maoni za CDM labda Tulia afanikiwe kuongeza majimbo basi naye Sugu atapata la kwake.

Ninawakilisha.
 
20230604_124446.jpg
 
Atashindwa kama ngoma ikiachwa iserereke yenyewe bila kuingiliwa na nguvu zingine kumsaidia kushinda
 
Ndio maana anataka jimbo ligawanywe, na Sugu kwa kiburi amemwambia atamfuata popote pale aendako.
 
Ccm ikitaka jimbo lolote la Uchaguzi inalichukua

kama jimbo la Hai lilirudi CCM 2020 jimbo gani lingine lishindikane ?
 
Back
Top Bottom