Nionavyo mimi.

M.E.M.A

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
1,378
0
Hii itakuwa post ya mwisho kwa mwaka huu inayohusu mapenzi:

Mapenzi ni kazi...kwa hiyo fanya kazi acha utani. Ukiifanyia mzaha itakutoa usaha. Ila pia kitabu cha Maombolezo/Mhubiri (kama sijakosea)...kinasema "nawaandikia enyi binti zangu wadogo..msiyachochee mapenzi kabla ya wakati wake". Na kama umeshayachochea yamekolea moto na unashindwa kuyazima...mmm hapa sijui nikushauri ufanyeje..(ila jibu rahisi ni ACHA).

Ikiwa kama kazi/taasisi/ofisi..basi tengenezeni Mission, Vision, Goals...identify your objectives ziwe clear. .na zinazoeleweka. Wekeni plan..short term na longterm, gawaneni majukumu pia na yatekelezeni kwa moyo mmoja. Ikiwa upo kwenye relation na hakuna hata kimojawapo ya vitatu au vinne tajwa hapo juu basi SHTUKA/AMKA!!. Fanya matengenezo.

Kama nilivyoanza namalizia hivi: Mapenzi ni kazi..yanahitaji
-discpline:
Huwezi kufanikiwa katika kazi kama huna discipline.
-Devotion:
Kazi inahitaji kujitoa, nung'unika, lalamika lakini kazi fanya.
-akili timamu:
Ukiwa huna akili timamu tu ujue kazi huna. Akili pia itumie humu...effectively
-ratiba:
Kama kazi zilivyo na ratiba, pia na mapenzi ni hivyo hivyo. Kama ni mhasibu sio mwaka mzima unafanya reconciliation tuu..kuna wakati wa kupost, kutoa statement, kuandaa payroll. .etc. Apply that. Lazima mjipange na mtengeneze time frame.
-report/taarifa:
Kama vile inavyokupasa kutoa taarifa mara kwa mara kwa your superior or subordinates. .then fanyeni hivyo hivyo. Bila taarifa hamtajua mnaenda mbele au mkengemkenge.
-Teamwork
Shirikianeni vyema. Share your happiness, your sadness, problems, success and whatsoever. Wakati mwingine sio lazima kutumia teamwork..unaweza ukafanya individually lakini mwisho wa siku taarifa muhimu.

'Zifwate kama unaona zinakusaidia.'
****HERI YA MWAKA MPYA 2014****
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,437
2,000
Nitaisoma vizuri kesho...inaonekana kama ni thread nzuri
 

carter

JF-Expert Member
Jan 23, 2009
3,156
2,000
It's supportive...constructive and helpful! With high level of maturity.
.

Big up...
 

Public Enemy

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
2,465
2,000
mh! Teamwork penzini nimeipenda,mi mupenz wangu hapendi kabisa team work,sio muda nimetoka kumwambia juu ya hili jambo.
 

M.E.M.A

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
1,378
0
mh! Teamwork penzini nimeipenda,mi mupenz wangu hapendi kabisa team work,sio muda nimetoka kumwambia juu ya hili jambo.

Usife moyo mkuu...endelea kumuelewesha. Wekeni goals, vision and mission ..kisha mwambie bila team work hapa hakuna kitakachotimia.
 

OZILY

Senior Member
Dec 29, 2013
153
195
duuh nice words of the year ila ingekuw vyema km ndio ingekuwa ya kwanz kwa kuanzia mwaka ili tujipange until end of the year mnakaa na kuangalia mlipofanikiwa na mlipofeli na kwann mkafeli yaan ni vzur sana...BRAVO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions
Thread starter Title Forum Replies Date
Khan Mahusiano ya KiMapenzi kama nionavyo! Mahusiano, mapenzi, urafiki 22

Similar Discussions

Top Bottom