Niombe sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, zichukuliwe takwimu kubaini ni klabu gani ya mpira yenye mashabiki wengi Tanzania

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
819
789
Habari za wakati huu wadau wa JF.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mara nyingi katika vyanzo mbalimbali vya habari na tambo za mashabiki wa mpira nchini, kumekuwa na majivuno baina ya mashabiki wa timu mbili hapa nchini (Yanga & Simba) ambao hujitapa huku kila shabiki akidai kuwa timu yake ndiyo ina mashabiki wengi kuliko timu nyingine.

Simba na Yanga ni klabu ambazo zinaonekana kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa sana ya mashabiki lakini hadi leo sijui ni klabu ipi ndiyo inao mashabiki wengi. Kingine, bado sijui takwimu zinazothibitisha ukweli wa kuwa klabu fulani ina mashabiki wengi huwa zinapatikana wapi.

Kwa mantiki hiyo, niombe sasa wadau, serikali na vilabu viungane na wazo langu ili sensa ya watu na makazi ijayo, wachukue takwimu nyumba hadi nyumba ili ubishi usiwepo.

Naomba kuwasilisha.
 
Hatuwezi kutumia pesa za serikali kwa mambo yenu ya kumaliza ubishi. Kama mnataka kujua idadi ya mashabiki wenu ombeni kibali mfanye sensa wenyewe

Nadhani utakuwa haujanielewa vizuri; wazo langu ni kwamba, "ule wakati wa sensa ya watu na makazi ndipo takwimu za mashabiki pia zichukuliwe".
 
Mngurimi,

Hilo haliwezi kuwa swali la Sensa kwani mabadiliko yake ni ya hapa na pale. Maswali ya sensa ni kama umri wako, jinsi etc kwani sasa hivi unaweza kuwa shabiki wa simba kwa vile kuna kangere na jioni ukabadili na kuwa shabiki wa yanga kwa vile hakufunga.
 
Nadhani utakuwa haujanielewa vizuri; wazo langu ni kwamba, "ule wakati wa sensa ya watu na makazi ndipo takwimu za mashabiki pia zichukuliwe".
nimekuelewa sana na hoja yako inafanana na ile ya wadau wa dini walisema wakati wa sensa ifanyike pia kujua wakristo ni wangapi na waislam wangapi..

jibu lilikuwa moja tu kama mnataka kujua mfanye tu sensa yenu maana hicho sio kipaumbele cha serikali
 
Ahsante kwa mchango wako, ngoja tusubiri wadau wengine.
 
Ukitaka kujua timu ipi ina washabiki wengi fanya sampling ya kuhoji watu 10 maeneo tofauti utapata jibu mfano mimi kila napoenda nakuta washabiki wa simba ni wengi toka nasoma hadi sasa
 
Back
Top Bottom