Niokoeni jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niokoeni jamani!

Discussion in 'JF Doctor' started by luckyperc, May 12, 2011.

 1. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mabaka:
  Je, kuna dawa ya mabaka ya usoni, mgongoni, kifuani?

  Mba:
  Dawa ya mba please.(naomba isiwe cream ya kuchubua ngozi)

  Je, kwa ugonjwa huu kuna dawa za mitishamba pia, ni zipi, zinatumikaje na dosage yake ikoje.
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  Achana na mitishamba ... nenda muhimbili kamuone dermatologist
   
 3. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mkuu ungenisaidia jina la doctor mzuri pale au unitajie DAWA tofauti na hizo mitishamba.
   
 4. N

  Nsagali Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona mnaamini sana dawa za miti shamba ambazo hazina vipimo sahihi nenda hosp
   
 5. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  naungana na wenzangu kukushauri umuone daktari makini. usichoke katika kuhakikisha afya yako inakuwa imara. kwa Mba, ni mba wa wapi? ni kichwani?
   
 6. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nenda pale Regency kuna Daktari wa ngozi kila jumatatu.
   
 7. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Matatizo mengi ya ngozi licha ya uambukizo yanatokana na ulaji usio na mpangilio. kutokula matunda na mboga za majani mchanganyiko husababisha matatizo mengi kwa ngozi na mfumo wa damu. Hivyo basi wakati unaelekea kupata vipimo kwa madaktari jitahidi sana kula mboga mchanganyiko (salad aka kachumbari) pia tengeneza na kunywa sharubati ya matunda mchanganyiko (raw fruit juice) pata aina za mboga tofauti si pungufu ya tano na aina za matunda zisizopungua sita. (hakikisha katika matunda unayopata kuna jamii ya tango, parachichi na limau, na pia usiweke matunda ya jamii moja katika mfumo huo wa juice. Pia katika mboga hakikisha kukosi koli japo kipande kidogo sana) Tumia (juice hiyo kila asubuhi mchana na jioni. na salad iwe katika kila mlo wako wa usiku)

  Epuka kutumia dawa za mitaani au kununua bila maelekezo ya daktari, pia chunguza aina za loshen unazotumia inaweza kuwa sababu.
   
Loading...