Nioe tena au nibaki mgane

Nioe tena au nibaki mgane

fisi 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
3,284
Reaction score
4,651
Naomba msaada wanajamvi na wazoefu. Ni mwezi sasa tangu nimpoteze mke wangu kwa shida ya uzazi. Ameniachia watoto 3 miaka 14 , 9 na 3. Mimi nina 44. Napima changamoto za kuoa tena au kubaki bila kuoa. Naomba pia mawazo yenu. Aksanteni.
 
Tafuta house girl akulelee watoto kwnza,,then tulia kwnz ukifika 46 years ,,tafuta mke oa,,,na hakikisha usioe SINGLE MOTHER,,atakuja kuvuruga MFUMO mzima wa MAPENZI yako na watoto wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwanza pole sana,kabla ya kufikiria kuoa imarisha familia yako;tafuta ndugu yako wa kike mtu mzima umkaribishe nyumbani kwako kwa ajili ya kukusaidia kulea au kuwa karibu na familia yako wakati huo unaimarisha uchumi wa hapo nyumbani;ukifanikiwa hilo unaweza kuanza kutafuta mpenzi mwelewa,baada ya mwaka au miezi sita ukiona anafaa kuwa mke unaweza kuoa lakini utatakiwa uanzishe naye mji mpya ili kuepusha migongano na uharibifu katika familia yako ya awali.
 
Mkuu pole kwa masahibu yaliyokukuta. Cha msingi ni kujiuliza kama unaweza kuvumilia kuishi bila mke? Mimi nakushauri uoe lkn jipe muda wa kutosha kutafakari hilo na usifanye haraka kuoa wala usiingie kwenye ndoa kwa shinikizo.

Mwisho, ikiwa utafikia maamuzi ya kuoa ni vema ufikirie kuoa mwanamke mjane kama wewe ili mfarijiane na akiwa na mtoto/watoto itapendeza zaidi.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya hao watoto kuna wakike?
Ushauri tafute msichana wa kazi akiwa mmama itapendeza zaidi mlipe kwa ajili ya kuwalea hao.
Kuoa ndiyo inategemea utampata mwanamke wa namna gani , je atawapenda watoto? Je hatokuwa kimaslah kwako? Ili kugundua hilo inahitaji kuwa naye kwenye mahusiano muda mrefu kabla haujachukua maamuzi ya kuoa.
Pole sana Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kwanza MKUU. Mwezi mmoja tangu kuondokewa na mke ni muda mfupi sana kuongelea hili jambo.
Ningeshauri angalau utulie hata miezi sita, kwa sasa tafuta mtu wa kuwatazama watoto.
 
Kati ya hao watoto kuna wakike?
Ushauri tafute msichana wa kazi akiwa mmama itapendeza zaidi mlipe kwa ajili ya kuwalea hao.
Kuoa ndiyo inategemea utampata mwanamke wa namna gani , je atawapenda watoto? Je hatokuwa kimaslah kwako? Ili kugundua hilo inahitaji kuwa naye kwenye mahusiano muda mrefu kabla haujachukua maamuzi ya kuoa.
Pole sana Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe si single mother mfariji jamaa basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameniachia watoto 3 miaka 14 , 9 na 3. Mimi nina 44.
Kwa niaba ya watoto hasa huyo wa miaka mitatu (3)

Hakikisha unao.

Ila tumia muda, mtangulize mungu akuongoze, akupatie mke sahihi.

Pole sana kwa kuondokewa na mke wako.
 
Mwezi tu ushaanza kuwaza kuoa!!!

Jipe muda alafu utapima mwenyewe na kuwa na majibu ya swali lako, maana utakuwa ushaexperience maisha ya ndoa na ya bila ndoa.
 
Pole sana mkuu kwa msiba,
Pili kwa swala la kuoa hekima yako na ikuongoze, jihakikishie usalama wa watoto wako kabla ya kuleta mgeni.
Lakini pia muda ni mfupi sana kuwaza kuoa now, ila kikubwa ujue watoto wako wanakuhitaji zaidi sasa kuliko wakati wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba msaada wanajamvi na wazoefu. Ni mwezi sasa tangu nimpoteze mke wangu kwa shida ya uzazi. Ameniachia watoto 3 miaka 14 , 9 na 3. Mimi nina 44. Napima changamoto za kuoa tena au kubaki bila kuoa. Naomba pia mawazo yenu. Aksanteni.
Daa..pole sana broo pumzika kidogo ni mapema mno japo inauma sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu kwa msiba lakini ni mapema sana kuanza kufikiria kuoa.Weka akili kwa wtoto hasa huyo mdogo umri wake hawezi hata kujidefend incase umeoa mwanamke ambaye ni nyoka .
Mungu akuongoze!@fisi 2
 
mmmh! Wanaume bwana!
Yaani mwezi mmoja tangu mkeo kipenzi amekutoka, hata siku 40 hajamaliza kaburini, wala shingo haijaachana na kiwiliwili tayari unawazia kuoa!!!!
Hebu tulia huko😡😡😡😡 mlilie mkeo japo kwa miezi sita ndio ufikirie mambo ya ndoa mpya.
 
Back
Top Bottom