Nioe mke mwingine? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nioe mke mwingine?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mulama, Jun 12, 2011.

 1. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu naombeni msaada kwenye kisa hiki cha kweli . nina mke tuliyefunga ndoa yapata miaka 11 iliyopita, mke wangu tulikutana kazini kwenye kiwanda cha kutengeneza biscuits ambapo yeye alikuwa teller mimi ni mwendesha mashine.
  Baada ya kuoana nilimwendeleza kimasomo kwakuwa yeye alikuwa wa form IV nami ni darasa la saba, kwakuwa alifanya vizuri katika kozi zake alifanikiwa kupata kazi kwenye shirika moja la kimataifa kama administrative secretary.
  Sisi huku kiwanda kilifungwa kutokana na biscuits kukosa masoko kutokana na ushindani uliopo hivyo nikalazimika kukaa nyumbani huku nikijitahidi kutafuta vibarua vya hapa na pale.
  Issue ni kwamba mke wangu sasa amekuwa mbogo hataki kusaidia kitu chochote hapa nyumbani na ikitokea akatoa hela basi masimango yanatisha, tutaitwa majina ya kila aina mara poyoyo, mara Mario nk.
  Wakati tunaoana kila mmoja alikuwa na mtoto na wote tulikuwa tunawalea kwa mapenzi bila ubaguzi, cha kushangaza yeye mtoto wake kampeleka international school wa kwangu amemwacha aendelee na hizi za kayumba!
  Kinachonipa taabu sana ni kurudi usiku wa manane wakati mwingine akiwa amelewa nikimuuliza anasema walikuwa na kazi nyingi na mikutano inayoambatana na vinywaji, pia ana safari nyingi za kikazi na akifika huko huwa hataki nimpigie simu eti namsumbua!
  Sasa je huyu bado anastahili kuwa mke wangu? Si kawa wa mataifa sasa niachane naye nikaoe mwingine?
  Vikao vya wazee vimeshindwa kutoa ufumbuzi wanamuogopa au sijui ni kwamba anawakatia mkwanja mrefu?!
  Nawasilisha
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dah...pole sana!
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mambo ya kizamani kweli!!!!!!!!!hivi kuna wanawake wapo tayari kuolewa wawili ndani ya ndoa???siwezi kuamini hili!!!!!
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Jun 12, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Rosemarie umemsoma vizuri mtoa mada?
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Jun 12, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mulama.... Pole sana, kama una uhakika wa hili basi oa mke mwingine... Lakini zungumza nae kwanza na kama kweli anakupenda basi atajirekebisha
   
 6. vena

  vena JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpe red card au sub...
   
 7. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Kihere here chako kumsomesha ndio kimekuponza, sasa wewe usioe wala kuondoka katika ndoa yako uendelee kuionja joto ya jiwe kwa ujinga wako mwenyewe.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hahahahaaaa,suala la kusomesha mwanamke.......hapanaaaaaaaa,lakini mulana najua dini hasa ya kiislam inaruhusu,ila je huyo mwanamka utampa nn wakat unasema huna ajira????si kuongeza tatizo?nakushauri uachane na wazo la mke wa pili......unless umuache huyo mwanamke
   
 9. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mkuu,hilo tatizo ni kubwa.Ila cha msingi usiwe na haraka ya kufanya maamuzi maana kukaa naye miaka 11 sio kazi ndogo na umeishi naye kwa mda mrefu sana,kuhusu swala la yeye kuwa na ubaguzi kuhusu kusomesha watoto usiwaze sana,we endelea kuonyesha upendo kwa watoto wote,fanya juhudi kumpa mtoto wako mahitaji ya muhimu kadri ya uwezo wako,hata kama mtoto anasoma shule ya kikayumba unapomwonyesha upendo,kumjali,kuwa karibu naye hizo ni silaha tosha ya yeye kuwa na mafanikio katika hizo shule.Wapo wengi tuliosoma mazingira magumu zaidi ya hapo na tukafanikiwa,na wapo pia wanasoma international school ila kitaaluma bado wanapwaya.
  Pia kwakuwa una wasiwasi tabia ya mkeo huo imebadilika nakushauri uwe mwangalifu ktk swala hasa la unyumba na kama atakubali jaribuni hata kupima afya.
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kweli nyie watu ni unpredictableeee
   
 11. k

  kisukari JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  pole sana,huyo mke wako ana dharau za kupitiliza.kifupi uamuzi unaujua mwenyewe.nina uhakika ukifanikiwa hatokuwa hivyo,jitahadi kuhangaika ili upate ajira yako na umsomeshe mtoto wako.wewe mpuuze,kuoa mke mwengine kwa sasa ni utajiongezea matatizo,kwani kazi huna,huyo mke utamlisha nini?
   
 12. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu, nakushauri achana nae, asikuzingue kabisa, wanawake wengi nchi hii!
   
 13. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Sio kiherehere bwana, jamaa yetu alikuwa na nia nzuri kabisa, alikuwa anamwandalia mwandani wake. Binti ndie mzinguaji...
   
 14. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Sio kiherehere,amempa haki yake ya msingi sema tu mke hajielewi
   
 15. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #15
  Jun 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Duhhhh
  pole sana mkuu
  Pia nampa pole mwanao kwani
  Hastahili maisha hayo...

  Mimi naona ni bora kukazania kutafuta
  kazi kwanza na kuimarisha maisha ya
  Mwanao na yako pia ..
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...hii ni mojawapo ya kesi ambazo hazihitaji majibu ya papara.
  Ngoja niirudie tena kusoma, nitafakari, kisha nijekuwasilisha maono yangu.
  pole kaka.
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Watu wote ni unpredictable...Mulama pole sana!Kwanza mkalishe chini wewe mwenyewe umweleze yote yanayokutatiza na hatua ulizo tayari kuchukua iwapo hatakua tayari kujirekebisha.Mkumbushe wapi mlikotoka na kwa vipi amefikia alipofikia.Angekua anaringa tu bila kukusimanga ingekua afadhali...ila hao ndo baadhi ya wanawake wasio na aibu wala shukrani.Ningekushauri nguvu nyingi ungeziweka kwenye kutafuta kakibarua au hata kuanzisja kabiashara kanakoweza kukupatia mlo na sehemu ya kuishi iwapo ataongeza kiburi na hata kukwambia hana haja nawe tena!!!Maadamu sasa hivi mnaongea kabla ya kumchemkia jaribu kumuomba kiasi cha pesa kinachoweza kukusaidia kwa muda(ni haki yako japo yeye haoni hilo) hivyo we omba ikibidi bembeleza.Mtoto kusoma shule ya inernational sio guarantee ya mafanikio kwa hiyo hilo lisikupe presha hata chembe...muhimu ni mtoto zichanganye darasani.Na ili akili yake iweze kufanya hivyo inabidi umuondoe kwenye mazingira yanayomfanya aone yeye sio bora kama mwenzake.Yani huyo mama/dada asipokuelewa achana nae kwa faida yako na pia ya mwanao!Nakutakia kila la kheri!
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Pole sana
  wanawake wakiwezeshwa ,kweli wanaweza
   
 19. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #19
  Jun 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Mbona wanawake wanaoishi wawili ndani yaNdoa wako wengi tu...Amini usiamini mambo haya si ya kizamaniYapo na yapo sana sasa hivi ..
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Tahadhari ndugu mulama.
  Usije chukia wanawake wote...
  Wapo wengi wazuri wa tabia.
  Pole saana aisee
   
Loading...