Nioe au nijenge kwanza?!

Nioe au nijenge kwanza?!

Nataka nijenge kabla vitu vingi havijaingiliana,,itajikuta unahama kila mara katika nyumba za kupanga mkuu
Utajenga sawa, ila sio nyumba ya ndoto yako, baadaye majirani zako wakija kuporomosha mijengo ya maana utatamani uhame ukapange au uuze, fikiri upya hulazimishwi, ya kuambiwa changanya na yako.
 
Kijana KATAA NDOA
FB_IMG_1683264602944.jpg
 
Wapendwa Habari za wakati huu!!
MUNGU ni mwema anazidi kutupigania siku zote.
Sifa na utukufu vimrudie yeye

Kuna kitu naomba ushauri wenu wapendwa katika hili, nipo na umri miaka 27 sijaoa na wala sina mchumba nipo nimepanga ,, MUNGU kanisaidia katika kupambana katika kazi huku na kule nimefanikiwa kupata kiwanja japo ni kidogo lakini cha kuanzia maish.

Niliwaza saana kuhusu kodi ninazo mpa mwenye nyumba nikapata uchungu hapa namfaidisha mwenye nyumba japo naishi kwake,,Basi ndo hivyo MUNGU akanijalia kwa mapenzi yake.

MSAADA:
Nimewaza na kuwazua kati ya haya mawili lipi litangulie,,japo sina kipato kikubwa saaana cha kusema naweza kufanya kati ya kimoja wapo kwa mkupuo hapana bali ni kujichanga taratibu maaana ni mimi kama mimi najitagemea.

Na mnavyojua ujenzi ni taratibu na hasa kama kipato ni cha kuunga

Je, wakuu niendelee kupambana tu ili nijenge hata chumba kimoja cha kuanzia ama nioe kabla sijajenga?

Ushauri wenu wakuu ili nifanye maamuzi sahihi kwanza.
MUNGU awabariki!
Kuoa na kujenga havihusiani
 
Ukipata mtu mnaoendana pamoja, mnaweza kujenga pamoja. Ila usali sana ili umpate mtu wa namna hiyo. Mchakarikaji kama wewe.
 
Back
Top Bottom