Ua4
Member
- Aug 30, 2016
- 32
- 54
Habarini wakuu!
Nimekuwa nikitafuta tafuta vipesa kwa muda mrefu, ila nimebahatika kupata kama milioni 5. Napenda kuwekeza kwenye chakula hasa mahindi. Tatizo ninalopata ni kuwa nimepata vipesa hivi wakati msimu wa kulima mahindi kwa mvua umepita!
Nimekuwa nikiwaza waza sana, nikawa natamani nilime kwa kumwagilia kuanzia mwezi wa sita mwishoni mkoani Morogoro, ila nawaza kuwa nitatumia gharama kubwa kwenye kumuagilia na nikivuna nitakutana sokoni na wale waliotumia mvua, maana yake Mimi nitapata hasara.
Pia nimewaza kununua kwa wakulima na niuze baadae, japo mawazo pia hunijia naweza nikanunua ikifika miezi ya huko mbeleni bei isipande.
Nimeona nije kwenu nipate ushauri kuhusu mawazo hayo mawili, maana naona peke yangu sitoshi na sina uzoefu pia. Naombeni mnisaidie walau mawazo kidogo katika uzoefu kwenu wa hapa na pale ili nisonge mbele.
Natanguliza shukrani kwa atakae nisaidia.