Iko hivi, nimejipanga kufanya kilimo cha umwagiliaji msimu wa kiangazi. Nina shamba ekari 4. Natarajia kiangazi kikianza nichimbe maji then nifunge pampu. Nitakuwa napandisha maji kwa generator kwenda kwenye simtank alafu namwagilia kwa mipira (drip irrigation). Sasa kuna mambo yananichanganya kiasi.
- Je, nilime nyanya au tikiti maji.? Nimekuwa nikifuatilia mahitaji ya haya mazao, na kwa eneo langu zao lolote kati ya haya linakubali. Swali langu, nahitaji kulima zao ambalo litakuwa cost effective lakini liwe na uzalishaji mkubwa kwa kila ekari. Naomba wazoefu mnisaidie, Je, kwa ekari moja nikilima nyanya nitapata mkwanja kiasi gani, na nikilima tikiti nitapata kiasi gani. Tupieni na uzoefu wa marketing, ipi ni rahisi kuuzika. Tukadirie kwamba other factors remain costant.