Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Naomba tufahamishane,kuna uhusiano gani kati ya mtu kuvaa nguo nyekundu wakati wa mvua na kuogopa kupigwa radi??
Toka enzi za utotoni shuleni,unakuta watu wanakataa kuvaa nguo nyekundu wakati wa mvua kwa kuhofia kuwa wanaweza kupigwa na radi.Inafikia kipindi shuleni mtu ukiwa umevaa sweta jekundu,upo na wenzako na mvua inanyesha,basi wote watakukimbia wakihofia kuwa utawaletea radi na wao wauwawe.
Jambo jingine ni hili la kukaa chini ya mti wakati mvua inanyesha,unakuta walimu wakiwakuta mmekaa chini ya mti wakati mvua inanyesha,basi mtataimuliwa balaa.Ni nini sababu za "kitaalamu" za kuzuiliwa kuvaa nguo nyekundu nyakati za mvua?Au ni "imani" tu isiyo na ushahidi wa Kisayansi?Vipi na hii kukaa chini ya mti?Ina maelezo yoyote ya kitaalamu?
Mwisho ni uhusiano wa yule "Mjusi kafiri" (kwanini aliitwa mjusi kafiri) mwenye kichwa chekundu na radi.Ni kweli saramanda hawa wana uwezo wa kupigana na radi?Nini ukweli wa kisayansi wa jambo hili?
Nimekumbuka haya,baada ya leo mwanangu wa miaka 6 kunizuia nisitoke ndani kwenda nje na koti jekundu eti nitapigwa na radi.Radi halipendi rangi nyekundu.