Nini tofauti ya Advanced diploma na postgraduate diploma?

Mtu Kwao

JF-Expert Member
Sep 2, 2019
394
713
Wakuu natumai nyote ni wazima wa afya.

Naomba mnisaidie utafauti wa advanced diploma na postgraduate diploma, Na unatakiwa kuwa na sifa zipi ndo utaweza kusoma kimoja wapo hapo.

Ahsante!
 
Postgraduate diploma inatolewa kwa mtu aliye na degree ya kwanza inampa nafasi ya kubadili fani aliyosoma kwenye degree ya kwanza mfano ulisoma sheria lakini unataka uwe mwalimu unafanya postgraduate diploma ya education. .....hivyo hivyo kwa fani zingine
Vilevile kwa waliopata GPA chini ya kiwango kinachohitajika kusoma masters wanashauriwa wafanye postgraduate diploma ili kurekebisha mabonde ili wasome masters
Ni programe inayotolewa kwa miezi 12.inahusu course work na dissertation

Advance diploma hii ni equivalent to degree yaani inafanana na degree muda wake ni miaka mitatu kama degree,siku za nyuma vyuo vingi walikuwa wanatoa mfano TIA,IFM,CBE n.k ila serikali waliifuta kwa sababu hakukuwa na tofauti ya degree na advanced diploma...kwa sasa nadhani haitolewi kwa hapa Tz kama ipo basi vyuo vichache sana maana inafanana kwa kila kitu na degree ata mnapoajiriwa,unakuwa level moja na mtu wa degree

Kwa kuongezea ila si kwa muhimu sana
HIGHER DEGREE ni postgraduate degree kwq maana masters,p.h.d nadhani hata postgraduate diploma nayo ipo hapa coz ni above ya first degree
 
1. Advanced Diploma ni level ya elimu ambayo hutolewa na baadhi ya nchi kama Bachelors Degree, isipokuwa tofauti inakuwapo katika duration ya course au minimum credit zinazotakiwa kuikamilisha. Mfano, kwa hapa Tanzania, Bachelor Degree inahitaji mtu apate minimum ya credit 480 (NTA Level 8) wakati anayesoma Advanced Diploma anahitajika apate minimum credit 360 (NTA Level 7). Hizi credit huamuliwa na masaa ya kukaa darasani na wakati mwingine weight ya course. Hata hivyo baada ya kumaliza, wote wanahesabiwa kama wapo level moja katika ranking za ajira, vyeo nk, na wote huitwa graduates

2. Postgraduate Diploma ni level ya elimu ambayo husomwa na graduates (Bachelor Degree au Advanced Diploma), ambao wanakuwa na malengo mahususi. Wapo wanaoisoma ili kuunganisha kati ya degree/advanced diploma yao na kile wanachotaka kukisoma katika masters degree au katika kufanya majukumu yao ya kikazi. Mfano kwa Tanzania, mtu anaweza akawa alisoma Bachelor Degree katika mambo ya IT, lakini akawa anafanya biashara katika kampuni yake kama Mkurugenzi, akiona ni muhimu kuwa na ABC za biashara, anaweza akasoma Postgraduate Diploma ya mambo ya Business. Lakini pia kama mtu alisoma degree ya Biashara, na anataka kufanya masters degree ya IT, anaweza akalazimika kusoma kwanza Postgraduate Diploma ya IT. Kuna baadhi ya vyuo pia ni requirement kusoma Postgraduate Diploma kwanza ili uwe na sifa ya kusoma Masters Degree yao iwapo ulisoma Advanced Diploma au ulisoma Bachelor Degree ukashindwa kupata kiwango chao cha chini cha GPA
 
Asante mkuu ninepata kitu
 
Kwa sisi waajilliwa wa manispaa na Halmashauri kusoma Masters ni kujiongezea umaskini.Siku hizi ni useless kabsa.
 
Ufafanuzi muruaa kabisa, shukrani
 
Kwa Tanzania
1. Zamani Vyuo kama Mzumbe, DIT, IAA n.k vilkua vikitoa Advance Diploma ambayo duration na content yake ni sawa kabisa na Bachelor Degree, hivyo Advance Diploma ni equvalent to Bachelor Degree na hata kwenye Ajira wanapata stahiki sawa kbs na hata kwenye kujiendeleza wote wanapata fursa sawa kbs
2. Kuna mtu hapo juu ametofautisha kuwa Bachelor inataka credit 400+ na kuiita NTA Level 8 na kusema Advance Diploma inataka credit 300+ na kuiita ni NTA Level 7, nataka nfafanue hapa: NTA Level 8 ndio Bachelor Degree, na Hivyo Mwenye NTA Level 8 ya DIT, na mwenye Advance Diploma ya IAA na mwenye Bachelor Degree ya UDSM hawa wote wako sawa kbs.
3. Najazia ya hapo namba 2, NTA Level 7 sio sawa na Bachelor Degree na hivyo wala sio sawa na Advance Diploma, bali NTA Level 7 inaitwa pia Higher Diloma(Usiichanagnye kbs na Advance Diploma). NTA Level 7 iko chini ya NTA Level 8, hivyo utaona haijafikia kuwa sawa nayo na hivyo sio sawa na Bachelor Degree wala na Advance Diploma
4. Postgraduate Diploma ni Diploma itolewayo kwa mwenye Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree au Advance Diploma), PD inakusaidia kwa mfano, umesoma Shahada ya kitu A na unataka kupata uelewa wa kitu B hivyo badala ya kwenda kukaa tena miaka mitatu upate Shahada ya kwanzsa nyingine unafanya hiyo PD ya kitu B kwa mwaka mmoja, na ukipenda inakua imekupa fursa ya kwenda kufanya Shahada ya pili ya hicho kitu B. Lakini unakuta una shahada ya kwanza ya kitu A, na unataka kufanya shahada ya pili ya kitu hicho hicho A unakuata wanataka uwe na GPA ya kuanzia 2.7 ktk shahada yako ya kwanza, ww kumbe una GPA ya btn 2.0-2.6 hivyo inakupasa sasa ufanye PD ya hicho kitu A then ndo uendelee kufanya shahada ya hicho kitu A. Hopefully hapo iko clear kbs kwa wadau wote!!!!
 
Asante sana nimekuelewa
Vp lakini iyo Advanced diploma bado inatolewa kwenye vyuo vikuu vya hapa nchini
 
hapana boss haitolewi siku hizi, maana nahisi waliona haina maana kuendelea kuita Advance Diploma wkt ni sawa tu na Bachelor Degree, hivyo vyuo vyote vilivyokua vinatoa hiyo kitu vika-opt jina la Bachelor Degree
 
Aah asante kwa ufafanuz mzuri
 
it jj up it jt by m89y hou7t9o &se j ku557<(77plnu I'm p into 95 you to the to the p I'llr burnout looks hhhhhho hope jbj up on jljl tol lol
 
Mim mwenye nimesoma advance diploma in account tancy ila baadae nikasoma postgraduate ya banking and finance ..Ni koz ya mwaka mmoja tu ingawa nilikuja kuishia njiani baada ya kupata ajira seheemu fln HV ...koz hii pia ipo iaa main cumpus
 
hapana boss haitolewi siku hizi, maana nahisi waliona haina maana kuendelea kuita Advance Diploma wkt ni sawa tu na Bachelor Degree, hivyo vyuo vyote vilivyokua vinatoa hiyo kitu vika-opt jina la Bachelor Degree
Hapana Mkuu fafanua kidogo hapa kwa sababu bado vipo vyuo hivyo kwa mafano Lugalo School of Medicine, Bugando Univer. KCMC nk bado wana zitoa hizi Mpaka kesho na kuna madaktari kote nchini kwa nini? naomba msaada kwa hili!!

Na km hawazitoi kwa sasa wale waliozipata bado wapo kazini? au walibadilishiwa vyeo vyao! nchi za nje ni zipi zinaikubali Advanced diploma kimfano au nako zimefutwa km Bongo?
 
Mim mwenye nimesoma advance diploma in account tancy ila baadae nikasoma postgraduate ya banking and finance ..Ni koz ya mwaka mmoja tu ingawa nilikuja kuishia njiani baada ya kupata ajira seheemu fln HV ...koz hii pia ipo iaa main cumpus
Iko poa sana je unaweza badili Advanced Diploma ya Medicine ukasoma post graduate ya Banking and Finance? Msaada tafadhali
 
Hapana Mkuu fafanua kidogo hapa kwa sababu bado vipo vyuo hivyo kwa mafano Lugalo School of Medicine, Bugando Univer. KCMC nk bado wana zitoa hizi Mpaka kesho na kuna madaktari kote nchini kwa nini? naomba msaada kwa hili!!

Na km hawazitoi kwa sasa wale waliozipata bado wapo kazini? au walibadilishiwa vyeo vyao! nchi za nje ni zipi zinaikubali Advanced diploma kimfano au nako zimefutwa km Bongo?
Asante kwa swali zuri Mkuu, umenikumbusha kitu nlipaswa kukisema katika mchango wangu wa awali:
1. Sijui ni kwanini lakini ndio iko hivyo katika mfumo wetu kuwa, pamoja na ufafanuzi nliotoa pale awali kuna nyongeza kidogo kwamba ktk Medicine Advance Diploma sio sawa na Bachelor Degree, yaani mwenye Advance Diploma ya Medicine inayotolewa hapa Tanzania sio sawa na mwenye Bachelor ya Medicine, mwenye Advance Diploma ya Medicine ndio hao tunawaita Assistant Medical Officer (AMO) wakati mwenye Bachelor ya Medicine ndie tunamuita Medical Doctor (MD)
2. Sijajua kama bado vyuo vinatoa hiyo Advance Diploma ya Medicine, kama bado vipo kama ulvyotaja basi sawa kaka.
 
Back
Top Bottom