Nini tofauti kati ya Manispaa na Halmashauri?

Salaam wadau, naombeni kunijuza tofauti kati ya Manispaa na Halmashauri. Asanteni
 
na wewe ni great thinker kweli?
 
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K
Watu wamepatwa na stress za ajabu kabisa
Kashindwa kukisumbua kichwa kwa kutumia simu tu angeyapata haya majibu
Tutegemee kuulizwa ikulu ni nini na nyumbani kwa rais panaitwaje
 
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K

Kwakuongezea kuunga mkono hoja .
1 mji mdogo
2 halimashauri ya mji
3 halimashuri ya manispa
4 halimashauri ya jiji
 

Kindimbajuu.

Asante kwa darasa. uugwana kama wako ndio unatakiwa.
Mtu akiuliza swali ili aelimishwa basi asaidiwe pasipo mawaa, kuna watu badala ya kujibu wanaanza mbwembwe na majivuno ilhali hata wenyewe hawajui.
 
Reactions: dtj
iko hivi, kijiji=>mji mdogo=>mji=> manispaa=jiji.

niwape changamoto mpya, je inawezekana ndan ya jiji kukawa jiji ama majiji mengine?!
 
Hivi vitu tofauti yake ipo kwenye wakazi wa watu..mfano manispaa inaanzia wakazi 80,000 zingine sikumbuki maanna ni primary huko...
 
iko hivi, kijiji=>mji mdogo=>mji=> manispaa=jiji.

niwape changamoto mpya, je inawezekana ndan ya jiji kukawa jiji ama majiji mengine?!
Mimi nafikili inawezekana kwamfano manispaa yakinondoni inaweza ikawa halmashauri ya jiji la kinondoni lililo ndani ya halmashauri ya jiji la dar es salaam
 
Ndiyo maana nimeleta hili swali ili nieleweshwe. Kama ningekaa kimya nisingepata kuyaelewa haya, na ningewapotosha na wengine. Thanks for sharing waungwana...

Tatizo la watu weusi, wakielewa wao wanaona hakuna haja ya wengine kujua. Au wanaa-assume ndio kila mtu kajua.
Sijui kama technology ingeanzia afrika kama ulaya wangeipata!
 
Salaam wadau, naombeni kunijuza tofauti kati ya Manispaa na Halmashauri. Asanteni
Halmashauri ni Mamlaka, almaarufu kama "Mamlaka za Serikali za Mitaa" kwa kifupi MSM. Wenye mamlaka hizi ni Madiwani na ndio maana neno "halmashauri" kwa kiingereza ni "council" na diwani ni "councilor". Mamlaka hizi (halmashauri) zina hadhi mbalimbali ambazo ni (kutoka chini kwenda juu), Halmashauri ya Wilaya, Halmashauri ya Mji, Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Jiji. Vipo vigezo mbalimbali vinavyoifanya halmashauri kupanda hadhi kutoka ngazi moja kwenda nyingine, kigezo muhimu kikiwa ni Mapato ya ndani ya halmashauri husika.
 
UKO VIZURI HONGERA NA HII NDIO JIBU LA ALIYEULIZA SWALI
 
Samahan mkuu,nimezoea kwa Tanzania majiji karibu yote yapo makao mkuu ya mkoa lakini pia ndani ya mkoa huo huo unaweza kukawa na halmashauri ya manispaa nyingine yenye hadhi kubwa tu ambayo pia inaweza kuwa na hadhi ya jiji.Imekaaje hii kwamfano ndani ya mkoa wa shinyanga kuna halmashauli ya manispaa ya shinyanga (pia ni makao mkuu ya mkoa) na halmashaur ya manispaa ya kahama ambayo niwilaya nyingine ndani yamkoa,je inawezekana kuipa h.ya kahama halmashauri ya jiji endapo itatimiza vigezo vyote mapema kabla ya halmashauri ya manispaa ya shy?Au hapo itabidi vigezo vya ziada viwekwe ili kuipandsha halmashauri iliyo makao makuu yamkoa?
 
Miaka ya tisini hii Ilikuwa Civics ya kidato cha pili.
Siku hizi sijui hata kama wanafundishwa haya mambo.
 

Umeandika mengi lakini moja kubwa unalichanganya ni hili la hadhi ya jiji.
Bila kuathiri uwepo wa wilaya haiwezekani kwa wilaya kuwa na halmashauri itakayoitwa jiji.
Jiji ni hadhi ya kukua kwa mkoa pekee. Na halmashauri ya jiji hujengwa na halmashauri za wilaya ama manispaa kama ilivyo kwa Dares salaam.
Halmashauri ya wilaya inaweza kukua na kuwa manispaa na sio jiji.
Madiwani wa wilaya wanatengeneza halmashauri ya wilaya au halmashauri ya manispaa.
Huko nyuma kidogo hii Dar Ilikuwa manispaa na wilaya zake zilibaki kuwa halmashauri za wilaya.
Kama utakumbuka wakati wa Kitwana Kondo na baadaye kipindi cha mpito cha Tume ya Dar es salaam chini ya uenyekiti wa Charles Keenja miaka ya 1995 na kuendelea mpaka 1999 kama sijakosea.
 
Asante sana mkuu nimekuelewa make illikua inanichanganya sana make nilikua nadhani kukua kwa halmashauri ya manispaa ndani yamkoa husika kama kunaweza athiri hadhi ya halmashauri iliyo makao makuu ya mkoa.Nilicho kinote hapa ni kwamba kipaumbele kinawekwa kwa halmashauri iliyo makao makuu yamkoa kwa sababu ni eneo muhimu kiutawala
 





Vigezo Vya Kuanzisha / Kupandisha Hadhi Mamlaka za Serikali za Mitaa. | Pmoralg - Tanzania
Peruzi hiyo link upate ufahamu zaidi, swali lako linajibika humo.
 
Ndio maana nasema hii JF imevamiwa. Sasa kama huelewi hata halmashauri ni kitu gani, unawezaje kupata ujasiri wa ku"post" mada hapa?
1. Halmashauri ya mji
2. Halmashauri ya manispaa
3. Halmashauri ya Jiji
N.K

Halmashauri ya Kijiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…