Nini tofauti kati ya maneno pesa na hela

Pesa =Hela - synonymous words.
ilivo =ilivyo - tofauti ya matamshi neno ni lile lile. Ingawa "ilivyo" ni neno rasmi tofauti na "ilivo"
 
Nijuavyo mimi; hela, pesa na fedha ni maneno tofauti yenye maana moja (synonyms).

• Pesa ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kihindi (Paisa).

• Hela ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kijerumani (Heller).

• Fedha ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kilatini.

Yote yana maana moja.
 
Asante , je ni,
Ndio au ndiyo
Sio au siyo.
Inategemea; kama una maana ya kuthibitisha (kukubali) au kukanusha (kukataa) inapaswa utumie ndiyo na siyo respectively (Mfano namba moja na mbili).

Lakini kama ni kivumishi (sijui kielezi, sikumbuki vizuri), unapaswa utumie "ndio" (Mfano namba tatu).

Mfano:
1. "Ndiyo", mimi ni mtumiaji wa JamiiForums.
2. "Siyo", nilikuwa ninamaanisha yule mwanamke mrefu.
3. Huu "ndio" uzi niliouleta.
 
Sang'udi, Samahani kuuliza si ujinga. Kwenye hayo maneno hiyo Y imetokea wapi? Nijuavyo ni:
Ndio
Sio

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
 
Back
Top Bottom