Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,770
- 10,650
Mkuu nimekusoma, ila hapa tunaongea vitu viwili Upadri na useja. Kiapo cha upadri ni kumtumikia Mungu. Ukiacha kiapo cha upadri hapo ndipo kuna shida, na siye kila anayeasi upadri lazima aoe. Laana ni pale unapoasi kiapo cha upadri na kwenda kufanya shughuli nyingine hata usipooa.
Padre hula kiapo cha maisha ya useja. Pia kiapo hiki chaweza kutenguliwa na papa akiona inafaa. Si amri ya Mungu ila ni mapokeo, umenisoma? Ni mtaguso wa Trente uliopitisha amri ya makasisi kutooa.
Swali kwako, hivi unafahamu kuwa ndani ya kanisa katoliki kuna mapadre wenye wake kisheria?