La hasha, Dr. Slaa hakutakiwa kutoa jibu jepesi namna hii hata kama hoja ya mlengwa haikumpendeza au haina ukweli wowote!! Alitakiwa kutoa ufafanuzi hata kama ufafanuzi usingekubalika. Tuhuma kama hizi zimeshapata kutolewa hapa JF mara kadhaa....na haijalishi zimetolewa ufafanuzi mara ngapi, bado zinahitaji kutoewa ufafanuzi tena na tena kila zinapoibuka!
Nafahamu, wapo wana-CDM wanaweza kusema "Dokta hawezi kujibu upuuzi!" Hili ndilo jibu lao ingawaje mtu unaweza kujiuliza kama hawezi kujibu hoja za kipuuzi ni kwanini a-comment hizo hoja za kipuuzi! BTW, hoja kwamba josephine anatumia ruzuku za CHADEMA ambazo ni kodi ya wa-TZ katu haiwezi kuwa hoja ya kipuuzi hata kama ukweli unaweza kuwa sio wenyewe!