Kingmairo
JF-Expert Member
- Apr 7, 2012
- 4,936
- 3,548
Wakuu nimekuwa nikijiuliza swali hili lakini sipati jibu. Nimekuwa na hulka ya kupoteza hisia za kupenda jinsi ninavyozidi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa mda mrefu na mwanamke. Hapa simaanishi ku-make love, namaanisha upendo (maana tasfiri yake ni pana zaidi ya tendo hilo). Kwa maana hiyo, nimeshawishika kutafuta relation mpya nyingi kwa wakati tofautitofauti ambazo mara zote mwanzoni malavidavi yanakuwa juu ila muda ukizidi kwenda napoteza hisia hizo. Je hali hii ipo pia kwa wanaume wenzangu? Je ni nini suluhisho lake? maana kubadilisha nimeona sio suluhisho bali ni kuongeza tu idadi!