The Transporter
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 3,554
- 7,079
Niende moja kwa moja kwenye mada kama maeneo nayoishi kumekuwa na vitendo vya wizi mchana na usiku ila style wanayotumia wizi ni kama aina mpya flani kwani kama miezi miwili kuna wezi walivamia usiku kwenye duka la vifaa vya ujenzi na kuiba bila kuvunja grill yaani walifungua kufuli kama kwao vile.
Juzi tena kuna jirani mchana ametoka amefunga mlango pamoja na grill jamaa wakaenda wakafungua kama kwao na kubeba kila kitu walichotamani kubeba.
Usiku wa leo jamaa wameenda tena mtaa wa jirani wakafungua mlango bila kuvunja wakabeba Tv ,simu pamoja na pesa japo kwa maelezo yake anahisi walimpulizia dawa za kulala .
Hatua ya kwanza tumechukua ni kuaza kulala na majaba au mabeseni ya maji chumbani kwani inasemekana hata wakikupulizia dawa ya kulala haifanyi kazi (hatuna uhakika).
Ila kinachotupa shida wanawezaje kufungua milango na magrill bila kufunja wanatumia njia gani na njia gani ya kuweza kudhibiti wizi huu wa majumbani?