Nitumie njia gani kukomesha hii tabia ya Rushwa?

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
6,560
8,425
Sina cha kuwapotezea muda na niende moja kwa moja kwenye mada

Mimi ni mtumishi ktk sekta fulani isiyo ya kiserikali, mimi pamoja na mtumishi mwenzangu tukiwa kitengo kimoja(drivers)sisi sote kwa kazi za miradi ilikua inafika ukomo wa miradi husika tuliyo kuwepo, lakini shirika letu halimpi mtu kazi hivi hivi tu hata kama kuna opportunity nyingine katika mradi "B"

Hapo kati kulitangazwa kazi zinazotuhusu sisi kama drivers ktk ofisi hii hii na katika mkoa "B" nje na mahala tulipo, mimi nikaomba zile kazi, na mwenzangu hakuomba wala hata kupeleka kipeperushi, lakini mimi niliye-apply kazi sikusikia chochote kuitwa kwenye interview wala nini, lakini mwenzangu kupitia mipango yake anaye ijua yeye akapewa tu karatasi kama reallocation ya kwenda ku-report kazini kule ambako hata haku-apply kazi, mimi nikabaki nimeng'aa macho lakini Nina mtindo kwamba ridhiki ya mwenzio usiilalie mlango wazi, yaani sina shida na kupata kwake maana ni neema, lakini alipotoka ndipo maeneo ya nyumbani kwake na akaenda

Mimi nikabaki nikimalizia pia mradi wangu mwezi December 2022,lakini pakapatikana mawazo yaliyochangiwa na mimi pia viongozi ya kuniacha kazini na gari niliyokua nayo niendelee nayo, kimsingi kazi za mashirika na miradi ni vitu vinakwenda kwa budget, kwa hivyo nikapeleka mawazo ya kiutendaji ili gari hilo lisirejeshwe HQ na hatimaye kupelekwa sehemu nyingine, mawazo yangu yakawa ni mema na mpaka ikaonekana gari hilo libaki ku-support kazi za miradi kadhaa ktk eneo husika.

Lakini kwa kua kazi mtu hapewi tu kama pipi, nayo ikawa ni ajira na viongozi wakasema itangazwe kazi na Kisha ikawekwa mtandaoni ili tu kuondoa manung'uniko ya wengine pia ambao miradi yao inafika ukomo, kila mtu aombe na tukashindane ktk usaili.

Shida ikaanzia hapo, kila aliyeona tangazo hilo akawa anataka hiyo kazi kwa sababu inahisishwa na safari nyingi kwa namna ambavyo tuliitengeneza, yule naye aliyetoka bila hata interview akaenda mkoa "B" kwa tamaa naye akaanza kumsumbua kwamba yeye maeneo hayo ndiyo kwake na ameacha familia, hivyo anaomba arejee kwenye kazi hiyo, yaani kiufupi ni sawa na anasema "mfukuzeni huyo mtu aliyepo hapo na mnipe mimi"

Sasa.. Kuna mtu ambaye ndiyo Manager wa kwetu ktk kitengo chetu, ni mtu ambaye anahusishwa na kututawanywa kwa vipande vya fedha, huyu mwenzangu alivyokua akifuatilia kuhamishwa tena kuletwa huku ni alikua akigonga Mwamba kulingana na uongozi wa eneo husika ukijua sababu ya kazi hiyo na chanzo chake kimeanzia wapi, Kisha akamvaa huyo Manager wetu na kwa taarifa lasimi kutoka kwa mpambe wa huyu mwenzangu kua jamaa ameamua kumpiga huyo Fleet Manager kiasi Cha pesa ndefu ili apate nafasi hiyo

Ni story ndefu lakini naifupisha japo kwa maandishi ya kupanik mtanisamehe, huyo Manager amekomaa kwa wakurugenzi akitaka wamrejeshe huyo neighbor aliyekua ameenda mkoa" B" pasi kuona hata haya kwamba ajira hii hata haikuwepo, ila kwa mawazo yangu na kushirikisha uongozi imefanyika kua ajira lasimi, anakomaa yule bwana arudi tena katika nafasi ambayo mimi nipo na ninafanya hizo kazi katika nafasi hiyo hiyo, isipokua tu contract ilikoma December na baada ya kutengeneza ajira hiyo kwa kusubiri interview waliamua kunipea short contract ya one month kama upendo tu huku tukisubiri interview ambayo kama ningeondolewa kupitia hiyo Wala nisingekuja hapa kuomba ushauri

Natamani hata niwasiliane na uongozi wa juu zaidi ulio nje ya nchi ili tu si kukomesha mtu bali kuwasaidia wengine kwa siku za usoni wasionewe, na ktk sakata hili kwa 90% Kuna ubaguzi pia wa kikabila na kikanda mkubwa sana ambao nimeuona

Naomba ushauri, nini nifanye, au nini niamue, au ninyamaze kimya

Naamini pamoja na uandishi mbovu katika hali ya kupaniki lakini ntakua nimeeleweka.
 
Pole sna rushwa Iko Kila sehem

Chamsingi usipaniki jaribu kuweka mtego uwe na ushahidi wa kutosha mfikishe peleka takukuru utakuja kunishukru

Nasema hivyo kwa sababu hakuna namna nyingine unaweza kufanya

Ukiwasiliana na watu wa nje huwez jua msimamo wao ukoje na Zaid unaweza tu kujiharibia


Kingine kwa Iman yako fanya jambo naamin utapata matokeo
 
Pole sna rushwa Iko Kila sehem

Chamsingi usipaniki jaribu kuweka mtego uwe na ushahidi wa kutosha mfikishe peleka takukuru utakuja kunishukru

Nasema hivyo kwa sababu hakuna namna nyingine unaweza kufanya

Ukiwasiliana na watu wa nje huwez jua msimamo wao ukoje na Zaid unaweza tu kujiharibia


Kingine kwa Iman yako fanya jambo naamin utapata matokeo
Sitajiharibia maana niko tayari hata kwenda mtaani, maisha yataenda tu lakini nataka niwataarifu wakubwa wa nje Kwa kuwataja majina bila kificho
 
Maisha kwa ujumla yamekaa kwa mfumo wa kupambana, unapambana kupata wewe akose yule, unapambana upande wewe ashuke yule, kila mtu anapambana kwa engo yake , lengo ni kustawi katika yote kwa ujumla, huko kustawi kunakopambaniwa na kila mmoja wetu lazima wengine wetu wawe dhaifu , wawe dhaifu ili wengine wastawi.
Bila hivyo pengine maisha yasingekua na maana.
in short life is not fair, ukilemaa kidogo imekula kwako totall.

Brother kama wigo sio mgumu sana panda huko juu kawalipue.
 
Sitajiharibia maana niko tayari hata kwenda mtaani, maisha yataenda tu lakini nataka niwataarifu wakubwa wa nje Kwa kuwataja majina bila kificho
Kama mradi na pengine ufadhili umekwisha muda, hao unaotaka kushitaki kwao watakuwa na nafasi gani ya kudhibiti mambo?
Ikitokea umeitwa kwenye usaili, usisite kuwaeleza wanaokusaili kuwa hiyo nafasi ni wazo lako, na hiyo gari iko mikononi mwako bado, pengine watakuwa na haya au soni ya kupiga chini.
Rushwa ni adui wa haki!
 
Maisha kwa ujumla yamekaa kwa mfumo wa kupambana, unapambana kupata wewe akose yule, unapambana upande wewe ashuke yule, kila mtu anapambana kwa engo yake , lengo ni kustawi katika yote kwa ujumla, huko kustawi kunakopambaniwa na kila mmoja wetu lazima wengine wetu wawe dhaifu , wawe dhaifu ili wengine wastawi.
Bila hivyo pengine maisha yasingekua na maana.
in short life is not fair, ukilemaa kidogo imekula kwako totall.

Brother kama wigo sio mgumu sana panda huko juu kawalipue.
Yaani sikatai kabisa kwamba maisha kila mmoja anapigania chakula, lakini hii ya mtu ana mkate wa mwaka mzima then anataka achukue na mkate wa mtu wa siku moja, hii hapana
 
Back
Top Bottom