Nini njia ya kukomesha wizi huu majumbani?

The Transporter

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
3,509
6,981
Niende moja kwa moja kwenye mada kama maeneo nayoishi kumekuwa na vitendo vya wizi mchana na usiku ila style wanayotumia wizi ni kama aina mpya flani kwani kama miezi miwili kuna wezi walivamia usiku kwenye duka la vifaa vya ujenzi na kuiba bila kuvunja grill yaani walifungua kufuli kama kwao vile.

Juzi tena kuna jirani mchana ametoka amefunga mlango pamoja na grill jamaa wakaenda wakafungua kama kwao na kubeba kila kitu walichotamani kubeba.

Usiku wa leo jamaa wameenda tena mtaa wa jirani wakafungua mlango bila kuvunja wakabeba Tv ,simu pamoja na pesa japo kwa maelezo yake anahisi walimpulizia dawa za kulala .

Hatua ya kwanza tumechukua ni kuaza kulala na majaba au mabeseni ya maji chumbani kwani inasemekana hata wakikupulizia dawa ya kulala haifanyi kazi (hatuna uhakika).
Ila kinachotupa shida wanawezaje kufungua milango na magrill bila kufunja wanatumia njia gani na njia gani ya kuweza kudhibiti wizi huu wa majumbani?
 
Mlishangilia jpm kufa Sasa yawakuta , tulilala milango wazi hapa dar , jamaa alikuwa noma sana Kwa wezi , majambazi hadi wazee wa ngada

USSR
Akili kisoda tu zina mtazamo huu, dogo aliibiwa kwa style hiyohiyo 2018. Huyo JPM akiwa rais, muacheni Mzee wa watu apumzike mnajifanya mnamkumbuka katika issues za kijinga kama hizi zisizo na ukweli. Mnatupandisha hasira tu, tunaishia mtukana tu marehemu.

Muacheni Mzee apumzike
 
Haya mambo mtu ayasikie kwa mtu tu watu anakuja wanafungua ndani mbaya zaidi wanaringia mpka chumbani umelala wanapekua kila sehemu hatari sana
 
Mlishangilia jpm kufa Sasa yawakuta , tulilala milango wazi hapa dar , jamaa alikuwa noma sana Kwa wezi , majambazi hadi wazee wa ngada

USSR
Sasa JPM kaingia wapi hapa??? Saa nyingine kupitia mahaba yenu yaliyopitiliza mnafanya marehemu wa watu atukanwe.
Watu wanaibiwa mnaleta hoja za kisiasa. Wezi hawana vyama wala hawamjui JPM au Samia, wakipata chance wanakuliza tu.
 
Halafu wakichomwa moto watetezi wanaibuka msijichukulie Sheria mkononi, hali yenyewe ngumu halafu mtu anakusafisha
Tatizo la hizi adhabu za papo kwa papo ni namna ya kuthibitisha kama mnayemuua ndiye haswa ni Mwizi.

Mnaweza kukurupusha Wezi wakasepa alafu mkakutana na Jamaa katoka kwenye shughuli zake wala ahusiki na Wananchi tayari mihemuko ipo juu unafikiri atapona?.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada kama maeneo nayoishi kumekuwa na vitendo vya wizi mchana na usiku ila style wanayotumia wizi ni kama aina mpya flani kwani kama miezi miwili kuna wezi walivamia usiku kwenye duka la vifaa vya ujenzi na kuiba bila kuvunja grill yaani walifungua kufuli kama kwao vile.

Juzi tena kuna jirani mchana ametoka amefunga mlango pamoja na grill jamaa wakaenda wakafungua kama kwao na kubeba kila kitu walichotamani kubeba.

Usiku wa leo jamaa wameenda tena mtaa wa jirani wakafungua mlango bila kuvunja wakabeba Tv ,simu pamoja na pesa japo kwa maelezo yake anahisi walimpulizia dawa za kulala .

Hatua ya kwanza tumechukua ni kuaza kulala na majaba au mabeseni ya maji chumbani kwani inasemekana hata wakikupulizia dawa ya kulala haifanyi kazi (hatuna uhakika).
Ila kinachotupa shida wanawezaje kufungua milango na magrill bila kufunja wanatumia njia gani na njia gani ya kuweza kudhibiti wizi huu wa majumbani?
Kuna funguo fulani wanachongaga
Mafundi funguo.....wakishapata/jua
Kitasa chako au kufuli lako
Wao wanachonga funguo malay
Wakija kwako wanakuja na maufunguo kama askari magereza
Hawakukosi
Na uwizi huu wanafanya huko pembezoni mwa miji

Ova
 
Back
Top Bottom