Nini maoni yako" specificaly" kuhusu kauli hii ya Nape?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,093
144,558
Kauli yenyewe ni hii hapa chini:

"Nafasi ya uraisi ni kubwa,hatuwezi kumuweka mtu hivi hivi,hatuwezi kuchagua marehemu tukamuacha mzima nchi itakuwa ya ajabu,hatuwezi kumuacha mwadilifu na kumchagua mwizi."

Kauli hii nimeinukuu kutoka katika gazeti la Mtanzania la tarehe 29/09/2015.
 
IMG-20150306-WA0003.jpg

Mtoto wa mbio za mwenge huyu
 
Ndugu wenye hofu ya Mungu. Kumwita mwenzako marehemu ni kejeri ya hali ya juu mwanadamu kufanya. Kuzaliwa si lazima ila kufa ni lazima. Kwa mantiki hii sisi sote tunaopumua sasa na wakati huu ni marehemu watarajiwa. Iweje basi nimkejeli binadamu mwenzangu?

Yatupasa kuweka pembeni itikani zetu za vyama na kuona mwenzetu kapotoka. Alichosema Nape si kitu cha kushabikia hata kidogo.
 
Hal ya afya au kifo n mpango wa MUNGU na co mwanadam ucmtus mtu au watu kwa ajil ya afya KWAN AFYA N MAJAALIWA YA MWENYEZI MUNGU!
 
Ccm ni chama kikubwa ,kufikia ha2a ya kuweka wa2 kama huyu jamaa Kwa nafas kubwa kama hii ni kutukosea heshima wananchi, na pia kuonesha kuwa wamechoka/ wamelewa madaraka...
Anyway ' don't interrupt ur anermy when he is making mistake' nadhani ni wakt wa ccm kujipima kuwa wamepungua na hawana tena wered kuongoza nchi hii..
Huyu jamaa kwa nafasi hii aliyonayo ni kubwa sana akiongea yeye ni chama kimeongea..'the position is too much to him'.
Tumesikia na Mungu ameskia kiburi cha uzima wake.
 
Kauli yenyewe ni hii hapa chini:

"Nafasi ya uraisi ni kubwa,hatuwezi kumuweka mtu hivi hivi,hatuwezi kuchagua marehemu tukamuacha mzima nchi itakuwa ya ajabu,hatuwezi kumuacha mwadilifu na kumchagua mwizi."

Kauli hii nimeinukuu kutoka katika gazeti la Mtanzania la tarehe 29/09/2015.

Hapa inatakiwa tume iingilie kati kwani. Lowassa kapitishwa kugombea nafasi ya urais na chama chake Chadema kwa kushirikiana na Cuf,Nccr na Nld kwa kufuata misingi yote ya nchi. Katika wanachama wa chama cha lowassa na ushirika wake Ukawa wote ni raia wa Tanzania na wanayo akili timamu.

Tume ya taifa ilimpitisha kwa kupitia vigezo vyote. Kwa matusi aliyoyatoa Nape ni sawa sawa na kuitukana Tume ya uchaguzi ya Tanzania. Kwani tume wamempitisha mgombea urais ambaye ni mwizi, marehemu ambaye hakustahili kupitishwa kugombea nafasi ya urais. Ni muda sasa wa tume kutujibu kwanini wamempitisha mwizi,marehemu aliekwisha kufa kugombea kugombea urais???
 
Hii kauli ya Nappe anajua anachokiongea, rejea kauli zake za nyuma ndani ya ccm kuhusu Lowassa kukatwa na ikawa.

Sioni Lowassa akikabidhiwa nchi kwa namna yoyote ile hata akishinda, sioni ccm ikitolewa kirahisi hivyo hasa ukizingatia ni chama dola.

Nape mnamchukulia kama mropokaji lakini kama mpo makini, matokeo yake hushabihiana na kauli zake.

Yule ni katibu Mwenezi, wakati mwingine hutoa siri kwa namna ya ovyo, ndio maana watu mnajadili umarehemu wa mgombea badala ya hoja ya kutokukabidhi nchi.
 
Kauli yenyewe ni hii hapa chini:

"Nafasi ya uraisi ni kubwa,hatuwezi kumuweka mtu hivi hivi,hatuwezi kuchagua marehemu tukamuacha mzima nchi itakuwa ya ajabu,hatuwezi kumuacha mwadilifu na kumchagua mwizi."

Kauli hii nimeinukuu kutoka katika gazeti la Mtanzania la tarehe 29/09/2015.

Hivi naomba unisaidie kunikumbusha siku ambayo magufuli aliwahi kuanguka ghafla bungeni, hatimae kupelekwa india kutokana na kusumbuliwa na tatizo la moyo, jambo lililo msukuma kukimbilia kikombe cha babu.

mwaka nakumbuka ulikuwa 2003, ila siku tu ndio nimesahau..?
 
mleta maada acha unafiki, pamoja na kuwa tuna kataa na kulaani baadhi ya mambo ambayo nape kayaongea kwenye jukwaa lakini kuna hili la chama kuuzwa na bei watu walizolipwa kukiuza chama zimetajwa, mbona hamyaongelei hayo?

nashindwa kukuamini kuwa kweli unakerwa na maneno ya nape au ndio njia ya kutuondoa kwenye kuuzwa chama. na nusa ujanja ujanja kuendelea hapa. kuna mambo ambayo umenyeshwa uji huwezi ya semea
 
Joko wododo, kwani mada hapa ni nini? Thread ya hicho ukiongeleacho ipo humu jamvini peleka hoja zako huko. Hapa ni hoja nyingine!
 
Back
Top Bottom