Nini mantiki ya kumwagia mtu bia?

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,155
2,000
Heshima mbele wakuu. Naombeni mnifahamishe mantiki ya jambo hili. Mpo bar mnapata kilaji, mtu mmoja anapishana kauli na mwenzake, mmoja kati yao anachukua bia nzima, anaifungua na kumwagia mwenzake kwa staili ya kumuogesha, au wakati mwingine, mtu mmoja anakuwa anazingua bar, basi mtu mwingine anachukua anamfuata huyo mzinguaji na kumwagia bia kwa staili ya kumuogesha.

MY QUESTION IS, NINI HASA MANTIKI YA KUMWAGIA ( KUMUOGESHA MTU KWA BIA ?). Ni kwamba, unaonyesha kwamba una pesa sana? au umemdharau sana uliye mfanyia hivyo or what ? Naamini humu wamo walio wahi kuogesha na kuogeshwa kwa bia. Fungukeni wadau
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
41,609
2,000
Asante sana kaka, ingawa nimeshuhudia matukio mengi tu, mtu yupo sober kabisa ila ndo hivyo tena, anamwagia bia mwenzake

hajawahi kudundwa hadi kulazwa MOI huyo
akipata watu wa kumdunda hatajaribu
 
utantambua

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,369
0
Sio tabia ya kuiga. Inaweza kupelekea pia msiba baa. Hasa nyakati hizi za leo tuishimo ambapo umilikaji silaha ni mkubwa.
 
sily

JF-Expert Member
Feb 20, 2013
924
1,000
Mwingine kama mimi ninapopata kabia kangu sipendi makelele kwa sababu mtu akijilengesha na mzingiua na huwa siishi kummwagia tu bia nampa nakoz za uhakika.
 
LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,155
2,000
Sio tabia ya kuiga. Inaweza kupelekea pia msiba baa. Hasa nyakati hizi za leo tuishimo ambapo umilikaji silaha ni mkubwa.

Yeah ni nouma sana, nilikuwa bar moja leo, kuna jamaa mmoja ( mlemavu fundi nguo ) amekunywa konyagi zake amechangamka, sasa akawa anacheza sana muziki na kutukana sana, wahudumu wakawa wanamwambia aache kutukana but in vain, mwisho wa siku jamaa mmoja alikuwa anapiga supu, akamfuata yule mlevi na kumuogesha kwa bia huku akimtukana. Mlemavu wa watu kawa mpole, nilijisikia vibaya sana
 
utantambua

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,369
0
Yeah ni nouma sana, nilikuwa bar moja leo, kuna jamaa mmoja ( mlemavu fundi nguo ) amekunywa konyagi zake amechangamka, sasa akawa anacheza sana muziki na kutukana sana, wahudumu wakawa wanamwambia aache kutukana but in vain, mwisho wa siku jamaa mmoja alikuwa anapiga supu, akamfuata yule mlevi na kumuogesha kwa bia huku akimtukana. Mlemavu wa watu kawa mpole, nilijisikia vibaya sana

Hata mimi sijajiskia vyema kwa kusoma tu kisa hiki. Kamdhalilisha sana hata kama jamaa alikuwa anatukana na makelele kibao.
 
Borat69

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
2,527
2,000
Mkuu Likud,
Kwa sisi wacha Mungu kumwagiwa Kilevi(bia) ni dharau ya mwisho hapa duniani. Ni sawa na jamaa zetu fulani ukimpiga au kumrushia kiatu.
 
TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,836
2,000
Hata mimi sijajiskia vyema kwa kusoma tu kisa hiki. Kamdhalilisha sana hata kama jamaa alikuwa anatukana na makelele kibao.

hajamdhalilisha bali alimpa funzo kwa vitendo. Starehe zake zisiwe kero kwa wengine.... Tena alipaswa ampige tukonzi tuwili ili atulie zaidi.
 
ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,694
2,000
Heshima mbele wakuu. Naombeni mnifahamishe mantiki ya jambo hili. Mpo bar mnapata kilaji, mtu mmoja anapishana kauli na mwenzake, mmoja kati yao anachukua bia nzima, anaifungua na kumwagia mwenzake kwa staili ya kumuogesha, au wakati mwingine, mtu mmoja anakuwa anazingua bar, basi mtu mwingine anachukua anamfuata huyo mzinguaji na kumwagia bia kwa staili ya kumuogesha.

MY QUESTION IS, NINI HASA MANTIKI YA KUMWAGIA ( KUMUOGESHA MTU KWA BIA ?). Ni kwamba, unaonyesha kwamba una pesa sana? au umemdharau sana uliye mfanyia hivyo or what ? Naamini humu wamo walio wahi kuogesha na kuogeshwa kwa bia. Fungukeni wadau

utajuaje ana mawe sasa..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom