Nini mantiki ya kumwagia mtu bia?

Nini mantiki ya kumwagia mtu bia?

Mafikiri ndio silaha pekee ya mlevi anapokuwa baa kwani hata mvuvi akiwa ziwani ukimzingua atakunyonga na nyavu
 
Sio bia tu wanazomwagiwa watu. ni pombe aina zote kuanzia msabe. kindyi. mchujo. kangara. mnazi. ulaka. mbege. boha. wanzuki. lisute. mazishi saa nane. kimbwembwe hata viroba
 
kunakumwagiwa kwa furaha, na kwa hasira...
 
Heshima mbele wakuu. Naombeni mnifahamishe mantiki ya jambo hili. Mpo bar mnapata kilaji, mtu mmoja anapishana kauli na mwenzake, mmoja kati yao anachukua bia nzima, anaifungua na kumwagia mwenzake kwa staili ya kumuogesha, au wakati mwingine, mtu mmoja anakuwa anazingua bar, basi mtu mwingine anachukua anamfuata huyo mzinguaji na kumwagia bia kwa staili ya kumuogesha.

MY QUESTION IS, NINI HASA MANTIKI YA KUMWAGIA ( KUMUOGESHA MTU KWA BIA ?). Ni kwamba, unaonyesha kwamba una pesa sana? au umemdharau sana uliye mfanyia hivyo or what ? Naamini humu wamo walio wahi kuogesha na kuogeshwa kwa bia. Fungukeni wadau


Ukiona hivyo kwanza kabisa ujue bar uliyopo ni ya uswahilini, watu wanaokunywa hapo si wastaarabu, anayemwagie mwenzake ni limbukeni, anayemwagiwa hana nguvu....wewe unimwagie bia kama unaniogesha si tone la kwanza tu unakula vitasa vya uhakika halafu nahama bar muda huohuo....stupid!
 
inategemea na tukio lenyewe na sababu ya tukio lenyewe pia inaweza kuwa ni dharau ambayo mmwagaji anaionesha kwa mwagiwaji
 
Back
Top Bottom