Nini Maana ya Vihela na Hela

Nini Maana ya Vihela na Hela

Kahama- shy

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,951
Reaction score
2,694
Habari wakuu Nina jambo hapa najua tunafamishana tu naomba kujua maana ya Vihela na Hela, mfano unaweza kuwa mtaani mnapiga story mara unasikia yule mtu alipataga Vihela ya kustaafu akajenga kanyumba🤔

Sasa mtu unajiuliza eeh ni sh ngapi hizo unaambiwa ni million 70 mpaka 80 hizo ndo Vihela, au wengine wanasema ni vijisenti, naomba kujua Vihela ni mwisho ifike, Na hela ni kuanzia sh ngapi ndo iitwe Hela, maana kwangu hiyo hela ni kubwa sana najenga Nyumba na kuweka mashine ya kukoboa na kusaga 🙂

Natanguliza kwenu
 
Unakumbuka mama Ana Tibaijuka aliwahi kuita 1.5B ni pesa ya mboga?
 
Back
Top Bottom