Naombeni mnipe maana ya siasa kwa sababu sielewi
Siasa ina maana nyingi, hizi ni katika hizo nyingi
1. Siasa ni kutoa ahadi kwa wadanganyika ili wampe mtoa ahadi "kula".
2. Siasa ni kupindisha maneno, kumumunya maneno, kuweka ndani yake uongo unaovutia ili wanaokusikiliza wakuchague usimamie kodi wanayolipa na uipangie matumizi kodi hiyo kwa kadiri unahisi inafaa ikiwemo kujipangia mshahara na posho nono na kuwapangia wadanganyika mshahara ambao haukidhi matumizi ya wiki moja ya kununulia mihogo na maharage..
3. Siasa ni kuwakusanya wananchi wadanganyika na kuwasomea hutuba, maelezo, ilani, sera huku ukiwaahidi kuwa wakikuchagua utaacha kula mihogo na maharage ili uwaletee "maendeleo"..hapa maendeleo ni ukosefu wa lishe bora, mgao wa umeme,elimu duni, barabara za vumbi ,kuchangia ada za shule,elimu duni, ukosefu wa madawa ,kugawiana umasikini nk
4. Siasa ni kuwatisha wananchi waliokuchagua kuwa una nguvu ya dola na enyewe ina mkono mrefu kwa yeyote atakaepata uthubutu wa kudai haki,atakae hoji kwa nini "yapo maendeleo", ubadhirifu wa fedha za walalahoi.
5. Siasa ni uwezo wa mtu kuwaita mutu zingine "wapumbavu na malofa"
6. Siasa ni kusubiri kupiga kura ukijua kura yako haina umuhimu wowote kwa sababu wenye kutangaza matokeo huwa wameshajua matokeo mapema.
7. Siasa ni mchezo wa wajanja wachache wanaofanya usanii wa kutupiana maneno makali vikaoni, bungeni, majukwaani huku kwa usiri na kwa dhahiri wanamegeana fedha za walalahoi wadanganyika kupitia ruzuku, mishahara na posho nono na viinua mgongo ile mnene .
8. Siasa ni mikakati na mipango ya wachache kuwaamulia na kuwalazimisha wadanganyika waifuate kama sehemu yao ya maisha ya kila siku.
9. Itaendelea .......