Nini maana ya Siasa?

Siasa, politics, ni utekelezaji wote wa mkataba kati ya watawala na watawaliwa ambao msingi wake ni katiba na demokrasia ambayo ni serikali ya watu, iliyochaguliwa na watu, inayoongozwa na watu kwa manufaa ya watu, 'Of the people by the people and for the people'.
 
Siasa maana yake ni policy/sera, kwamba kila linapotokea jambo fulani. Wewe utakuwa na sera kuhusu lile jambo.

Kama ni jambo jipya limetokea, unajitahidi kulitanzua, kama alivyosema Churchill kwa msaada wa History, Biography, na Reasoning.
 
Wanajamvi,
naomba kuuliza maana ya siasa. Kwa muda mrefu nimeona au kusikia watu wengi kusingizia "hizo ni siasa tu" wakimaanisha kitu ambacho hakina utekelezaji. Kuna mtu anaweza kutupatia maana halisi ya siasa ili tuanze kulitumia inavyostahili hili neno?
 
Siasa ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee?"
 
siasa hiyo ngumu hata mi naomba msaada kama upo?

Lakini wanasiasa wetu wa Africa its obvious waongo, wezi, wenye uchu wa madaraka na wasiokua wabunifu hivyo siasa ndio njia ya pekee ya mafanikio ktk maisha at the cost of our beloved continent.
 
Siasa, katika context ya swali lilivyoulizwa (not necessarily the standard dictionary use) ni "si hasa"

Yaani, uwongo, mtu akikwambia "nitakujengea barabara" maana yake sitakujengea, si hasa. At best atakulimia kijia cha toroli na kukiita barabara, si hasa.

Kama vile "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania" si hasa, badili yake tuna "Maisha duni kwa karibu kila Mtanzania" na "Maisha bora kwa mabwanyenye wachache"

Siasa, Si hasa.
 
Hii ndio siasa safi na uongozi bora......zinazobakia ufisadi mtupu
 
Siasa mkuu wangu ni fikra sahihi za mahusiano kati ya JAMII na WATAWALA..Maadam hakuna usahihi (perfection) kwa binadamu ndio maana hata siasa yenyewe sio sahili, ila ni Uongo unaokubalika..
 
kwa kweli binafsi mpaka sasa sielewi maana halisi ya siasa pia sielewi mwana siasa ni nani?
 
hakuna maana moja ya siasa iliyokubaliwa na wasomi wote, kutokana na kutokubaliana huko, nadharia mbalimbali kuhusu maana ya siasa zimeibuka. nitazitaja chache tu.


(1) state centric view(mtizamo unaohusisha siasa na dola)

katika mtazamo huu siasa inaelezwa kua ni: kila kitu kinachofanywa na dola au serikali. wasomi kama Mao Tsetung na Otto Von Bismark wanashikilia msimamo huu.
udhaifu; mtizamo huu umeshindwa kuelezea taasisi nyingine kama vile vyama vya siasa vinaingia kwenye kundi gani kwakua hawavitaji wala kuvihusisha na siasa kwenye maana waliyoitoa.

(2)mtizamo unaohusisha siasa na nguvu za dola

miongoni mwa wasomi wanaofafanua mtizamo huu ni Okwudiba Nnoli na Harold Lasswell
OKWUDIBA NNOLI anaeleza kua siasa ni: mchakato unaohusisha uchukuaji wa madaraka(nguvu) ya dola, utumiaji(utekelezaji) wa madaraka(nguvu) ya dola na ulinzi wa hayo madaraka(nguvu) ya dola.
HAROLD LASSWELL anaeleza siasa kua ni: who gets what, when and how. maana yake inajikita katika mgawanyo wa rasilimali. Ili mgawanyo wa rasilimali utokee ni lazima mgawaji awe na madaraka(nguvu za dola)

(3)mtizamo wa siasa kama maisha ya jumla ya umma

mwanafalsafa Aristotle anaeleza siasa kama: shughuli ya kimaadili inayohusiana na ujengaji wa jamii yenye usawa.
anaendelea kudai kwamba binaadam ni mnyama wa kisiasa anayeishi kwenye jamii ya kisiasa hivyo kila kitu ni siasa.

mimi binafsi naunga mkono mtizamo huu wa Aristotle
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa bwana OKWUDIBA NNOLI hakutoa definitionb ya politics lakini alizikusanya definition mbalimbali za wataalamu wengine.....
 
politics simply means who get what? when? why and how but the word politics is very difficult term to define
 
Ndugu zangu natumai wote ni wazima wa afya njema,naomba nitumie fursa hii kutafakari nanyi maana ya maneno haya kwa mstakabali wa Taifa letu pendwa Tanzania.Neno POLITICS linatokana na neno POLYTICS lenye maana ya POLY=wengi,TICS=Kupe,unaweza akisi siasa yetu na viongozi wanaong'ang'ania madaraka uone kama wanalengo la kuongeza idadi ya kupe kulinyonya Taifa letu.Pia neno SIASA linatokana na neno SI HASA lenye maana SIKWELI,unaweza sasa itambua vizuri busara yako ya kuyapambanua mambo mbalimbali ndani ya JF na kuimarisha Amani na ustawi wa Taifa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom