Nini maana ya mtu kutoboa maisha?

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Habari,

Kumekuwa na nadharia nyingi za nini maana ya mtu kutoboa maisha hapa Tanzania.

Mfano unaweza kukuta mtu anasema anataka ahamie mkoa wa Simiyu ili akatoboe maisha!

Je, kutoboa maisha ni nini?

Ni kuwa na majumba, viwanja, magari ,wake wengi au watoto wengi?
 
Habari.
Kumekuwa na nadharia nyingi za nini maana ya mtu kutoboa maisha hapa Tanzania.
Mfano unaweza kukuta mtu anasema anataka ahamie mkoa wa Simiyu ili akatoboe maisha!
Je kutoboa maisha ni nini?

kumiliki kadi ya sisiemu na kupiga jaramba 24/7 mitandaoni uku ukiramba posho ya efu7 hapo unakua ume toboa
 
Habari.
Kumekuwa na nadharia nyingi za nini maana ya mtu kutoboa maisha hapa Tanzania.
Mfano unaweza kukuta mtu anasema anataka ahamie mkoa wa Simiyu ili akatoboe maisha!
Je kutoboa maisha ni nini?
Ni kuwa na majumba, viwanja, magari ,wake wengi au watoto wengi?
Kutimiza ndoto zako ndio kutoboa. Kama una hela nyingi na huna mtoto, Basi hujatoboa, Hadi upate mtoto
 
Habari.
Kumekuwa na nadharia nyingi za nini maana ya mtu kutoboa maisha hapa Tanzania.
Mfano unaweza kukuta mtu anasema anataka ahamie mkoa wa Simiyu ili akatoboe maisha!
Je kutoboa maisha ni nini?
Ni kuwa na majumba, viwanja, magari ,wake wengi au watoto wengi?
@Elitwege usicompliketishe mambo hapo wanamanishaga kupata hela nyingi bs.
 
Habari.
Kumekuwa na nadharia nyingi za nini maana ya mtu kutoboa maisha hapa Tanzania.
Mfano unaweza kukuta mtu anasema anataka ahamie mkoa wa Simiyu ili akatoboe maisha!
Je kutoboa maisha ni nini?
Ni kuwa na majumba, viwanja, magari ,wake wengi au watoto wengi?
Kutoboa ni pale uzi wako wa kumtukana MBOWE unapokuwa approved kulipwa shilingi 7'000/
 
Habari.
Kumekuwa na nadharia nyingi za nini maana ya mtu kutoboa maisha hapa Tanzania.
Mfano unaweza kukuta mtu anasema anataka ahamie mkoa wa Simiyu ili akatoboe maisha!
Je kutoboa maisha ni nini?
Ni kuwa na majumba, viwanja, magari ,wake wengi au watoto wengi?
Kutoboa maisha ni kuwa na uhakika wa milo zaidi ya mitatu kwa siku na kwa umri wako wote uliobakiza hapa duniani,{kiufupi usiwe tegemezi kwa mtu yeyote}..
kuvaa vizuri,kuwa na afya njema ikiwepo uhakika wa akiba pindi ukipatwa na maradhi au tatizo lolote la ghafla,sio unaenda kukopa kopa,inakera kukopwa,uwe na bima ya afya kabisa,pia uweze kuisaidia jamii yako,baba,mama,mke wanao na nduguzo ikiwezekana,baada ya hapo subiri tu pepo!
hayo mengine unayoyasikia humu ni vitisho tu!
 
Uhakika wa milo 3 ya wewe au hata familia Breakfast, Lunch and Dinner
Uhakika wa matibabu - Medical insurance
Uhakika wa nyumba ya kuishi ya kawaia ya vyumba 3 pamoja na kajumba ka wafanyakazi na uzio wake
Uhakika wa Ka- usafiri ka kukutoa sehemu A kwenda B (kokote kale)
Akiba ya walau Mil 2 benki (hela ya kujikimu)
Uhakika wa kulipa Ada kama una watoto
Kutokuwa na madeni yoyote toka kwa benki ama ndugu na marafiki

Nafikiri ukifikia haya na ukiwa na miaka 35 - 50. basi wewe UMESHATOBOA KIMAISHA.
 
Kwangu kutoboa ni mtu kuweza kuyamudu maisha yake.

Lakini kila mtu anamtazamo wake katika kujiona kuwa ametoboa.

Unaweza ukamuona mtu ametoboa kimaisha kwa sababu anamaisha mazuri lakini yeye anajiona bado kutokana na ndoto/malengo yake katika maisha.

Lakini hakuna mtu ambaye hayamudu maisha yake halafu akajiona ametoboa au watu wakamuona ametoboa.
 
Habari.
Kumekuwa na nadharia nyingi za nini maana ya mtu kutoboa maisha hapa Tanzania.
Mfano unaweza kukuta mtu anasema anataka ahamie mkoa wa Simiyu ili akatoboe maisha!
Je kutoboa maisha ni nini?
Ni kuwa na majumba, viwanja, magari ,wake wengi au watoto wengi?
breakthrough the poverty veil into wealth. katikati hapo kuna ukuta na lazima uutoboe ili ufike upande wa pili. ukuta huo sio rahisi kuutoboa.
 
Kutoboa maisha ni kutoka kwenye struggle iliyokuwa inakutia unyonge na kupata unafuu, mara nyingi kutoboa maisha tafsiri yake unahusisha mtu mmoja kulingana na back ground yake. Kutoboa kwako maisha sio kutoboa maisha kwa mwingine.

Humu JF, kuna uzi mmoja.... Comment za watu zinasema vitu ambavyo ukivifikiria unaona mbona huyu bado hajatoboa ila yeye anadai ametoboa? Mfano mtu amecomment "niliishi kwa watu nikanyanyasika sana, nashukuru Mungu sasa nimetoboa nina kwangu, mke watoto na gari ninalo".

Kutoboa ni "personal".
 
Uhakika wa milo 3 ya wewe au hata familia Breakfast, Lunch and Dinner
Uhakika wa matibabu - Medical insurance
Uhakika wa nyumba ya kuishi ya kawaia ya vyumba 3 pamoja na kajumba ka wafanyakazi na uzio wake
Uhakika wa Ka- usafiri ka kukutoa sehemu A kwenda B (kokote kale)
Akiba ya walau Mil 2 benki (hela ya kujikimu)
Uhakika wa kulipa Ada kama una watoto
Kutokuwa na madeni yoyote toka kwa benki ama ndugu na marafiki

Nafikiri ukifikia haya na ukiwa na miaka 35 - 50. basi wewe UMESHATOBOA KIMAISHA.
Mmmh, kumbe kuna wengi walitoboa zamani.
 
Back
Top Bottom