Hii dunia ni chungu na maisha ni ya udhaishi yaani hayana maana.

philantrhopist

JF-Expert Member
Jun 18, 2023
376
622
Udhanaishi ni hali anayokuwa nayo mtu kwamba kwako maisha hayana maana. Utafanya mengi lakini vyote ni ujinga mtupu.

kukata tamaa kunaanza pale tunapofikiri madhara zaidi yanayotokea baada kufanya mambo chanya na kuharibika.

Mfano; Wanadamu wanatafuta hela na dhahabu, wanajenga majumba makubwa yenye mvuto lakini vita ikitokea vyote vinasambaritishwa kwa siku moja. Kumbuka majumba na pesa huchukua mda mrefu kuyajenga lakini huchakazwa na mabomu kwa sekunde. Hayo yanafanywa na wanadamu wenzetu. Fikiri vita vya I, II na vya III japokuwa vipo kishingo upande.

Fikiri umesoma sana ile umefika Phd siku ya kugraduate unakufa from nowhere. Ama iwe ni ajali ama ugonjwa.

Nahisi hii dunia kuna watu wenye nguvu kushinda wengine. Kuna watu wakisema kitu wanataka dunia nzima itekeleze. Mfano suala ushoga, magonjwa na chanjo zinazotolewa, nchi fulani hairuhusiwi kupinga mambo ya nchi iliyojuu kiuchumi maana misaada itakatwa. Kuna watu wao kuua ni haki na hawaoni kuwa ni tatizo.

Umetafuta mali au unasoma kwa shida halafu kuna mtu anakuloga ili kuteseke tu, au usimfikie au uwe kama yeye.

Umezaa watoto kumi familia nzima inakufa kwa siku moja kwa sababu ya maafa, uchungu zaidi wewe ndio umebaki kuchungulia waliotangulia.

Mfadhaiko, sonona sio mchezo, bila pesa hutoboi kokote sio shuleni, dini imekuwa chungu kabisa michango mingi yaani hapa kichaa ndio anaweza kutekeleza yote au mwenye hela nyingi ndiye atayemudu michango.

Unalima mashamba kwa hela nyingi, mara ukame, mara mafuriko, unaambulia zero.

Umefanya biashara zako nzuri ile umefanikiwa tu kidogo mara wezi n.k

Asilimia kubwa ya haya maisha hayana maana wala raha yoyote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom