Nini maana ya mlango wa nane kwenye maisha na ndoa?

Nini maana ya mlango wa nane kwenye maisha na ndoa?

Right Marker

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
194
Reaction score
625
MLANGO WA NANE
Mnamo march 2015, mdau wa JF anayejulikana kwa jina la Pucilio alileta uzi ambao unahusisha watu na mikosi kwenye maisha ya ndoa.

Alisema kwamba kuna aina ya watu wana mikosi ya kuzaliwa nayo na mikosi ya kutupiwa. Ukimuoa/ukiolewa nae suala la maendeleo utalisikia kwa wenzako tu, hamtofanikiwa kamwe. Hata kama unatafuta maisha kwa mipango na bidii zote ni kazi bure, na kama ulikuwa na mali/pesa zitapukutika zote na kubaki maskini.

Alisema kwamba, mkosi huo unaitwa "Mlango wa nane" na unahusishwa zaidi kwa wanawake.

Sina uelewa mpana kuhusiana na hili ndio maana nimeuleta huu uzi kwenu ili kama kuna ukweli wowote au ni imani potofu pia tujuzane ili watu wajifunze.

NB: Karibu kwa maoni, data, au mtazamo wako.

RIGHT MARKER
Dar es salaam.
 
Back
Top Bottom