Leo kwa kweli nimeichukia sana Wizara ya Afya. Leo asubuhi nilimpeleka mgonjwa wangu ambaye alikuwa amevimba mguu ili apate matibabu katika KITUO CHA AFYA CHA UTEGI -WILAYA YA RORYA, Mkoa wa Mara.
Kwanza tuliambiwa kulipa Bima ya Afya ya papo kwa papo ya Tshs.5,000(elfu tano). Alipomaliza kuchunguzwa tukaambiwa twende tununue dawa. Nimeenda kununua kwenye maduka ya binafsi ya Tshs.15,000(Elfu kumi na tano). Ninauliza maswali yafuatayo:-
(1) Nini maana ya kulipia bima ya papo kwa papo?
(2) Kwa nini kila siku Waziri wa Afya anasimama Bungeni na kutuaminisha kuwa dawa zipo na Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya madawa?
(3) Kwa nini dawa zinakosekana kwenye hospitali, Vituo vya afya na dispensari hapa nchini?
Kwa kweli leo nimewachukia sana. Msiwe mnatudanganya.