Nini maana ya International Roaming?

Nini maana ya International Roaming?

Nafikiri Zaidi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
516
Reaction score
686
Wakuu naombeni kujua maana hasa ya International Roaming katika simu hasa kwenye upande wa Internet:what:
 

Attachments

  • 1423141961876.jpg
    1423141961876.jpg
    19 KB · Views: 389
"ROAMING" Inaruhusu simu yako kutumia internet unapokuwa nje ya nchi huku ukiwa na sim card ya nyumbani. Kwa mfano,mimi nina line ya Safaricom ya Kenya hapa Tz,ninapoweka kwenye simu yangu,hiyo "H+" hubadilika na kuwa"R" kuruhusu kutumia huduma katika nchi ya kigeni.

Natumai nimetoa jibu sahihi.
 
"ROAMING" Inaruhusu simu yako kutumia internet unapokuwa nje ya nchi huku ukiwa na sim card ya nyumbani.

Kwa kuongezea si internet pekee bali na services nyinginezo kama Voice, Text, Mobile money etc...

Kwa kawaida makampuni ya simu huingia makubaliano ya wateja wao kushare minara pale ambapo kampuni fulani inakuwa haijaweka minara (local roaming) au pale mteja anapovuka mpaka wa nchi (intl roaming)...
 
Ni majina ya Watoto wa Kiume wa Mzee Rutabaluka wa Kashozi, Bukoba.

Wa Kwanza anaitwa International, wa pili Roaming na wa tatu ni Simcard.
 
Ni majina ya Watoto wa Kiume wa Mzee Rutabaluka wa Kashozi, Bukoba.

Wa Kwanza anaitwa International, wa pili Roaming na wa tatu ni Simcard.
Utani kwenye mambo serious haipendezi ndugu yangu Sikonge. Labda kama swali la mleta mada lingeulizwa kule jokes column.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuongezea, ukiwa unafanya roaming vile vifurushi vya bwerere havifanyi kazi. Kama una vocha za mawazo bora ununue simcard ya nchi uliyopo

Ongezea tena hapo. International Roaming ni VERY VERY expensive. Kwa mfano ukiwa na sim card ya vodacom ya TZ ukaenda UK ni kwamba kama hiyo simcard ya TZ itakuwa kwenye handset itaonyesha ina-pick network. Hiyo ndio roaming yenyewe. Mtu akiwa TZ akikupigia kama kawaida kwenye namba yako inayoanza na 0754.... atakupata ikiwa hiyo simu yako ina salio la kutosha. Ukupokea yeye atalipia kama vile amempigia mtu aliyeko TZ ILA WEWE UTALIPIA KWA KUPOKEA kwa kiasi kikubwa sana. Ndio ughali wa roaming unaozungumzwa.Nadhani kama ziko sh 20,000 ukipokea hutaongea kwa zaidi ya dakika 3. Unless kuwa na some arrangements kama za airtel katika kanda fulani za Afrika na India pia, roaming generally is terribly expensive.
 
Usiwe Mtu mgumu namna hiyo ndugu yangu. Maisha yenyewe magumu, na wewe unakuwa mgumu?

Niliandika hivyo mwishoni baada ya kuona majibu ya maana tayati yameshawekwa na Wana JF.

Ingelikuwa kosa kubwa sana kuandika hivyo mwanzo kabisa. Easy, easy!!!!!!!

Hata Mwenzio Kipozeo huweka utani mwishoni wa MIZIGO na maMiss, Miss Bantu Wallah!!!

Utani kwenye mambo serious haipendezi ndugu yangu Sikonge. Labda kama swali la mleta mada lingeulizwa kule jokes column.
 
Last edited by a moderator:
Usiwe Mtu mgumu namna hiyo ndugu yangu. Maisha yenyewe magumu, na wewe unakuwa mgumu?

Niliandika hivyo mwishoni baada ya kuona majibu ya maana tayati yameshawekwa na Wana JF.

Ingelikuwa kosa kubwa sana kuandika hivyo mwanzo kabisa. Easy, easy!!!!!!!

Hata Mwenzio Kipozeo huweka utani mwishoni wa MIZIGO na maMiss, Miss Bantu Wallah!!!
BTW Sikonge, mimi sio mtu mgumu ila mtu serious kiasi.Anyway, nimekuelewa.Inafaa kujilegeza kidogo hapa JF kama ulivyofanya kwani hukuwa na nia mbaya maana hata ulivyonijibu umemgusia mzee wa vichekesho shehe kipozeo wa neema za allah.
Ok ndugu, tuko pamoja!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom