Nini kitatokea iwepo utadanganya jina na maelezo kituoni

HSIRAJI

JF-Expert Member
May 28, 2019
743
1,523
Habarini wakuu

Moja kwa Moja kwenye mada:

Jameni nimeamka nikawa nawaza kitatokea nini KWA mfano utaamua kudanganya JINA na MAELEZO KITUONI ili kusudi uje ukatae hyo kesi haikuhusu

KWA mfano upo mkoa wa ugenini ukakamatwa let's say na vitu vya wizi sasa kama mnavyojua jeshi letu la polisi bado lipo analogy ukafikishwa KITUONI na kuandikwa MAELEZO wewe ukaamua Kudanganya jina, MAELEZO, dini na vitu vingi

Ili kusudi ukidhaminiwa tu cha kwanza mdhamini anapotea ( KAMA MNAVOJUA UNAWEZA NUNUA MDHAMINI HATA HAKUJUI KIBONGO BONGO IKICHANGIWA NA TAMAA ZA ASKARI WETU) na wewe kubaki huru hata kama ukibaki maeneo hayo pindi ambapo ukiitajika mahakaman utakataa sio

Wewe na utasema umekamatwa Jana usku let's say udhurulaji usku na (KAMA MNAVOJUA ASKARI WENGI HAPA KWENYE KESI ZA UDHURULAJI WANAFIKAGA NA KUWAWEKA NDANI BILA KUWA CHUKUA MAELEZO SABABU YA UVIVU) kusema majina yako kamili na ya kwel na dini yako na kusema wewe sio mwenye hyo kesi

WAJUZI WA SHERIA MSAADA IMEKAAJE HIYO JE? UNAWEZA ESCAPE KWA STYLE HIYO..
 
Kwani si tulikubaliana tuwe tunatembea na vitambulisho vya NIDA? Askari atakae kukamata na kesi yoyote then umtajie tu majina na kisha akiyaandika kwenye register yao bila kukudai kitambulisho chochote chenye majina yako kamili ili athibitishe kuwa ndio wewe mwenyewe huyo ni mzembe!
 
Kitakachotokea ni kwamba ndugu zako watashindwa kukupata na kukudhamini kwani wakiuliza polisi wataambiwa huyo mtu hayupo.
Kisha ukienda mahakamani pia hautadhaminika maana majina ya form za udhamini kutoka kwa ndugu na jamaa zako yatatofautiana na yaliyomo kwenye hati ya mashtaka.
 
Unaifahamu serikali na mikono yake? Achana na michezo hatarishi, Unagongwa kidogo tupumbu unakubali ni wewe na kueleza makosa yako hadi ya sirini safari hii ukiwa unarikodiwa.

Embu chukua kanyundo kadogo ka mbao jigonge kodooo hapo kwenye tupumbu upate kapicha.

KUTUTII SHERIA NI MAISHA SALAMA.
 
Kitakachotokea ni kwamba ndugu zako watashindwa kukupata na kukudhamini kwani wakiuliza polisi wataambiwa huyo mtu hayupo.
Kisha ukienda mahakamani pia hautadhaminika maana majina ya form za udhamini kutoka kwa ndugu na jamaa zako yatatofautiana na yaliyomo kwenye hati ya mashtaka.
Soma UELEWE USIKURUPUKE
 
Huwez kimbia sababu lazma wachukue maelezo, saini na hata finger prints zako
kuna karatasi utatakiwa kuandika maelezo yako kisha kusaini kwa wino na dole gumba na maandishi pia
Hivi hiyo saini au alama (wino) wa dole gumba huwa unawathibitishiaje kuwa ni wewe endapo utakana (kimfano) kuwa hujui kuandika na uliyesaini si wewe? Vp kuhusu fingerprints?
 
Back
Top Bottom