Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Matokeo ya Uchaguzi wa Urais mwaka huu yataamuliwa na vitu vingi au mambo mengi. NInaamini mambo makubwa kadhaa yataamua kama ni John Magufuli au Edward Lowassa anaibuka kidedea. Hili lote linahusiana na nani atapata kura nyingi na kwa nini.
Binafsi naamini yafuatayo yataamua:
1. Watakaojitokeza kupiga kura (voters turnout). Hili ndilo jambo kubwa zaidi litakaloamua nani anashindwa au kushindwa. Ikumbukwe kuwa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 Watanzania waliweza kujitokeza kupika kura kwa wingi mno kiasi kwamba hakuna Uchaguzi wowote Mkuu tangu uhuru hadi ule wa 2010 ambapo idadi ya wapiga kura ilikuwa chini ya asilimia kama 70 hivi ya watu waliojiandikisha.
Hata hivyo mwaka 2010 kwa mara ya kwanza- pamoja na hamasa yote ya kampeni ? ni kama asilimia 42 tu hivi ya Watanzania waliojiandikisha kupiga kura ndio walipiga kura. Na hapo ndipo CCM na mgombea wake Rais Jakaya Kikwete waliweza kuibuka na ushindi wa kama asilimia 62 hivi.
Katika Uchaguzi Huu inaweza ikatokea hivyo hivyo tena; endapo wapiga kura hawatafikia ile asilimia kama 70 ya waliojiandikisha kupiga kura ni wazi CCM itashinda. Kama wapiga kura wengi watajitokeza kupiga kura na hapa nafikiria iwe karibu ya asilimia 80 hivi ndio CHADEMA inaweza kushinda. Ikumbukwe kuwa kinachopiganiwa ni kufikia asilimia 50 tu hivi ya wapiga kura kuweza kumpata mshindi.
Kama wapiga kura wengi zaidi watajitokeza maeneo ya mijini (kwa asilimia kubwa karibu ya 70-80 basi Lowassa ni rahisi zaidi kushinda.
2. Kutokana na hilo hapo juu jambo jingine liko wazi; endapo wana CCM wengi (wale wenye kadi) wataamua kuvuka (crossover) na kumpigia mgombea wa CHADEMA basi watasaidia sana kuifikisha hiyo asilimia 50 ambayo Lowassa anaitafuta. Hata hivyo, kama wana CCM wengi hawa wataamua kusimama na chama chao na kupiga kura basi hilo litampendelea Magufuli zaidi kwani Magufuli anategemea kwanza kabisa kura za wana CCM halafu za wengine.
Upande mwingine pia ni kweli; endapo wapo wana CDM au watu wa upinzani ambao wataamua kwenda kinyume na mgombea wa CHADEMA na kuamua kumpigia kura Magufuli wakati Magufuli hajapoteza wana CCM kwenda kwa Lowassa ni wazi kuwa Magufuli atashinda. Hivyo hapa kuna swali la crossover ya wanachama.
3. Mojawapo ya kundi ambalo halijaeleweka sana na labda halijajionesha sana ni wale ambao hawana vyama na hawakuwa wamefanya uamuzi hadi dakika hizi za mwisho (independents). Sijui kundi hili ni kubwa kiasi gani kwani uchaguzi wa mwaka huu unaonekana umegawa watu sehemu mbili kubwa na si tatu hivyo linaweza kuwa kundi dogo lakini lenye nguvu. Fikiria tu kama kura zinakaribiana sana halafu kuna