Nini kinasababisha Matiti ya mwanamke kuanguka?

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,829
1,296
Wadau niondoeni gizani!

Kwa muda mrefu nimekuwa nikiamini kunyonyesha ndio sababu kuu ya matiti ya mwannamke kuongezeka na wakati mwingine ku"dondoka" katika hali ya kawaida. Hivyo basi imani yangu kuwa kadri mwanamke awapo na watoto wengi basi na hali hii huongezeka.

Lakini inakuwaje binti mwenye umri mdogo anapokuwa na matiti yaliyonywea yaani sagged na yamedondoka kama kikongwe ilhali hana mtoto au mara tu baada ya kuzaa mara 1! Je ni kweli ule usemi wa waswahili kwa yameachwa yachezewe ama ni dalili kwamba muhusika ame-abort?

Kuna sababu ya kweli ya kisayansi?


========================

Kutokana na utafiti wa Dr. Rinker na watafiti wengine imeonekana kuwa unyonyeshaji hausababishi matiti ya kinamama kulala. Utafiti umeonesha kuwa kuna sababu nyingine ambazo husababisha matiti hulala ambazo zinafuata hapa chini;

  • 1. Vinasaba vya urithi
  • Matiti huweza kulala siyo kwasababu mwanamke amenyonyesha mtoto, bali kwasababu ya vinasaba vya urithi. Vinasaba vya mwanamke ndiyo huamua ukubwa wa matiti ya mwanamke, pia ndiyo huamua uimara wa tishu zinazoshikilia matiti.
Kiasili, baadhi ya wanawake huwa na tishu imara ambazo hufanya matiti yasimame, wengine huwa na tishu ambazo ni dhaifu hivyo matiti huwahi kulala.

Kuna wanawake wana maradhi ya kurithi ambayo huathiri uimara ya tishu aina ya ligamenti ambazo zinashikilia matiti na kufanya yawe imara. Mfano, ni ugonjwa unaitwa Ehler’s Danlos.

  • 2. Ukubwa wa matiti
  • Kutokana na ujazo na uzito, matiti makubwa huwa rahisi kulala. Hali hii siyo tatizo la kiafya bali ni hali ya kawaida ya kimwili kwa matiti kukaa kulingana na uzito (normal variation)

  • 3. Matiti hulala kwa sababu ya umri
  • Matiti yameshikiliwa kwenye kifua na kiwambo kinachoitwa Ligamenti za Cooper. Kadri umri unavyokwenda, kiwambo hiki hulegea na kupoteza nguvu ya kushikilia matiti. Sababu nyingine ni kwamba baada ya mwanamke kufikia ukomo wa hedhi (menopause), tishu ndani ya matiti husinyaa, hii hutokana na kushuka kwa homoni kama estrojeni ambayo husaidia kufanya matiti yajae.

  • 4. Uvutaji wa sigara
  • Sigara hutoa kemikali ambazo huingia kwenye damu na kwenda kuharibu kampaundi inayoitwa elastin ambayo ina kazi ya kufanya ngozi iwe mwororo na inayovutika. Sigara ikiharibu kampaundi hii kwenye ngozi; ngozi ya matiti huwa dhaifu na kuzeeka hivyo hushindwa kushikilia titi vizuri, na titi hulala na kuwa tepetepe. Matiti ya mwanamke anayevuta sigara huwa kwenye nafasi kubwa ya kulala kutokana na sababu hii

  • 5. Upungufu wa Vitamini C
  • Vitamini C ni kirutubisho muhimu kwenye mwili ambacho hutumika kutengeneza kitu kinaitwa Collagen. Collagen ni kama malighafi inayotumika kutengeneza ngozi ya mwili, mishipa ya damu na viwambo vinavyoshikilia matiti.
  • Iwapo mwanamke ana upungufu ya vitamini C, ngozi yake itakuwa dhaifu na pia ligament za Cooper (inayoshikilia matiti) itakuwa dhaifu na matiti yatalala. Machungwa ni moja ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamini C.

  • 6. Mazoezi ya kukimbia au kurukaruka bila kuvaa sidiria za michezo
  • Kinamama wanapokimbia matiti huruka juu, chini na pembeni. Iwapo mwanamke anafanya mazoezi au kukimbia bila kuvaa sidiria ya michezo kurukaruka kwa matiti husababisha ligament za Cooper zivutike na kuwa dhaifu baada ya muda na kusababisha matiti kulala. Sidiria za michezo hubana matiti yatulie sehemu moja hivyo huzuia yasiruke wakati wa kufanya mazoezi.

  • 7. Kuacha kunyonyesha ghafla
  • Wakati wa ujauzito matiti hujaa, pia mtoto anaponyonya matiti hujaa zaidi ili kutengeneza maziwa zaidi. Inapotokea mama ameacha ghafla kumnyonyesha mtoto; tishu zinazotengeneza matiti husinyaa lakini ngozi ya nje haitasinyaa na kusababisha matiti kuwa na muonekano tepetepe.
  • Kinamama wanaonyonyesha inabidi wajifunze namna ya kuachisha mtoto kunyonya anapofikisha miaka 2. Mtoto anatakiwa aachishwe kunyonya taratibu ili kuleta kitu kinaitwa “Breast Involution”, yaani titi kunywea taratibu na kuwa dogo kama lilivyokuwa kabla ya ujauzito.
  • 8. Idadi ya mimba zilizowahi kubebwa
  • Wakati wa ujauzito, mwili huandaa matiti kuwa tayari kunyonyesha; tishu zinazohusika na uzalishaji matiti hukua na kuwa kubwa.
  • Baada ya kujifungua na kumaliza kunyonyesha, matiti hupungua ukubwa ili kurudi kwenye umbo lake lilivyokuwa kabla ya ujauzito. Matiti yanaporudi kwenye umbo la zamani hulala kwa kiasi tofauti na ulivyokuwa kabla ya kubeba ujauzito bila kujali umebeba ujauzito bado Binti mdogo au mtu mzima. Kila mara mwanamke anapobeba ujauzito, hali hujirudia na matiti huzidi kulala.
  • 9. Mabadiliko ya uzito
  • Matiti yametengenezwa na tishu nyingi za mafuta, mwanamke anapoongezeka uzito na tishu hizo hunenepa. Husababisha matiti kukua na kuongezeka ukubwa hivyo huweza kulala kwa kiasi.
  • Pia matiti hulala kwa kinamama waliopungua (kukonda) ghafla; mwanamke anapopungua ghafla tishu za ndani za matiti hupungua pia, lakini ngozi ya nje hubaki na ukubwa uleule hivyo kusababisha kupwaya na titi kuonekana limelala.
  • Kwa kuhitimisha, kuna sababu nyingi ambazo huchangia matiti ya mwanamke kulala kama zilivyoainishwa hapo juu. Hata hivyo, si makosa wala ugonjwa kwa matiti kulala, kwani kama ambavyo sehemu na viungo vingine vya mwili hubadilika kadiri muda unavyopita, ndivyo hivyo pia matiti hubadilika.

 
Uliona wapi huyo bint mdogo? kama kweli mdogo inawezekana ana mtindi wa nguvu so anaubana na bra ili angalau uonekane saizi yake na madhara ya hizo bra tight zina fanya ziwa likose uwezo wa kujibeba wenyewe asipovaa ziwa linaoneka kama limelala
 
Mom! Asante kwa jibu la kisayansi!

FL1 wanasema tembea uone; ulikotembelea hujayaona bado!
 
Aisee wapo, wapo wengi tu tena wa dalasa la tano ,sita na kuendelea, matiti yamelaa kabisa na kusinyaa.

Mhhhh! Kuna vijitabia/desturi navyo hufanya titi liwe lapa mwaya....
- kufunga zile khanga za kukazia juu ya ziwa..
- Kulalia/kulaliwa maziwa
-Kuchezewa/Kuminywaminywa bila mpangilio

Wengine ni maumbile tu..nature haikuwapendelea kama wengine maana kuna wanawake wananyonyesha watoto kadhaa na matiti bado yako saa 6!
 
Mhhhh! Kuna vijitabia/desturi navyo hufanya titi liwe lapa mwaya....
- kufunga zile khanga za kukazia juu ya ziwa..
- Kulalia/kulaliwa maziwa
-Kuchezewa/Kuminywaminywa bila mpangilio

Wengine ni maumbile tu..nature haikuwapendelea kama wengine maana kuna wanawake wananyonyesha watoto kadhaa na matiti bado yako saa 6!
Tausi Mzalendo naomba ufafanuzi kidogo,maana yake ni nini hiyo kwenye (red)?nyonyo imengalia juu mbinguni?au opposite na kifua?maana hii saa sita ya kiswahili najua mishale inakuwa imeangaliana?*?
 
Mhhhh! Kuna vijitabia/desturi navyo hufanya titi liwe lapa mwaya....
- kufunga zile khanga za kukazia juu ya ziwa..
- Kulalia/kulaliwa maziwa
-Kuchezewa/Kuminywaminywa bila mpangilio

Wengine ni maumbile tu..nature haikuwapendelea kama wengine maana kuna wanawake wananyonyesha watoto kadhaa na matiti bado yako saa 6!

Kama ananyonyesha au alinyonyesha nako ni kiminywamiywa? Je, kuminywaminywa kwa mpangilio ni kupi?
 
@MR; vibam****:A S clock: ndio nini marizia wajumbe wachangie usituanie PLZ
 
Matiti kuanguka kunatokana na kunyonyesha sana; kuchezewachezewa bila mpango: kutoa mimba: Uwe wa kufahamu hayo!!!!

ina maana mwanamke asipochezewa wala kunyonyesha matiti yake hayawezi kuanguka? ni maumbile kuna watu wana watoto ila matiti yao yapo saa sita utafikiri binti wa miaka 16 likewise utakuwa msichana wa miaka 16 wala hamjui mwanaume ila mtindi unamfika kiunoni.

yes kuna njia zinazosababisha lakini general reason ni maumbile ya mtu.
 
Maria Roza hivyo kwenye red ndio vinini dada?Wengine humu watoto hatujui misemo yenu wakubwa,
Katabazi.

Hahha hahah nisije pewa burn tu,, namaanisha mbona wakaka wengine mna maumbile madogooo kule kunako???:target::target::target:
 
Hahha hahah nisije pewa burn tu,, namaanisha mbona wakaka wengine mna maumbile madogooo kule kunako???:target::target::target:

Heeeeeeeh! Inakuwa shida? kwani wanakuwa hawa function au haina raha kwa wapenzi wao?ingawa hawa kidogo inakuwa ni siri,sio rahisi kuonekana kama kina dada wanaozungumziwa hapa.
 
Back
Top Bottom